HAKUNA LISILOWEZEKANA KWA MUNGU


Mtoto akiongea na Mtumishi wa Mungu Benny Hinny katika huduma ya miujiza huko Houston Marekani

Mtoto mdogo wa kike akiwa jukwaani. Mamake mzazi alishuhudia kuwa mtoto huyu alizaliwa njiti ikiwa alizaliwa miezi mitatu kabla ya miezi ya kawaida(yaani miezi tisa) akiwa mlemavu wa miguu. 

Madaktari walisema asingeweza kamwe kutembea na angekuwa na matatizo ya ubongo. 

Wakati mtoto huyu alipokuja kwenye huduma ya miujiza alikuwa hawezi kutembea wala kuongea vizuri, lakini wakati huduma ya uponyaji ikiendelea nguvu ya Mungu iponyayo ilimgusa kwa namna ya ajabu. 

Mtoto huyu alifuta machozi akimwambia Mchungaji Benny Hinny kuwa "Ninaweza kutembea sasa!" Mchungaji Benny alimshika mkono na kumtembeza chini na juu kwenye ngazi kitu ambacho mtoto huyu alikuwa hawezi kufanya hapo kabla.
Hakuna lisilowezekana kwa Mungu.

Comments