JINSI YA KUSIFU

ZABURI: Enyi watu wote pigeni makofi, mwimbieni Bwana.kwa kuwa bwana aliye juu ni mfalme wa yote atawatiisha mataifa chini ya miguu yetu.

Sababu za kumsifu Mungu:

1. Tunamsifu kwa vile alivyo. Ametukuka sana, ana nguvu.


2. Tunamsifu mungu kwa sababu ya matendo yake makuu.


Biblia katika Zaburi inasema Kwa kuwa Mungu ni mfalme mwimbieni kwa Akili, Paulo anasema imetupasa kuomba kwa Roho na kwa Akili pia. Nyimbo zinazotakiwa wakati wa sifa ni zile ambazo zinamsifu Mungu tu, na sio zilizokaa kama mipasho.
Pambio kama hizi za mipasho sio za sifa, pambio za sifa ni zile ambazo tunakuwa tukiimba kumsifu mungu, tukitaja sifa zake kama Ukuu wake, Uweza wake.

Kunatofauti katika Kuabudu na sifa isipokuwa zinashabiriana.
Kuabudu maana yake ni kuinama na kusujudu na kutukuza kitu kuwa hiki ni kikuu kuliko chochote, wimbo wa kuabudu sio lazima uwe wa taratibu.


Kuabudu ni kuinama na kumuinua Mungu. Zamani tulipokuwa tunaabudu tulikuwa tunanyoosha kabisa mikono, lakini siku hizi tunainua kwa imani tu .


Biblia inasema Maana Mungu ni mfalme inawapasa kumuimbia kwa akili: mambo haya hayatatimia kama hatufuati utaratibu ulio sahihi. 

KUOMBA:

Hutakiwi kukemea wakati wa maombi, unapokusudia kuomba ni lazima upeleke haja zako kwa Mungu. Lakini kabla hujapeleka maombi yako ni lazima kwanza umsifu mungu. Mungu atakuja upesi sana hata kama alikuwa na kazi ni lazima ataiacha na kushuka kwako, yaani kama ukianza kwa sifa utamshusha Mungu mzima mzima. 


Watu wengi hujali mahitaji yao, usichomeke mahitaji yako wakati wa kusifu. Bwana wetu yesu alitufundisha vizuri aliana kwa kusema baba yetu uliye Mbinguni Jina lako litukuzwe, ufalme wako uje…… na baada ya hapo akasema Utupe leo Riziki yetu, hapa sasa ndipo unaanza kuweka mahitaji yako. Pia kuna jambo la kusamehe, ni lazima kwanza umsamehe aliyekukosea, Yesu alitufundisha hivi: Utusamehe makosa yetu kama na sisi tunavyo wasamaehe waliotukosea.
 Kwa hiyo ukisha msamehe mwenzako ndipo sasa maombi yako yatakuwa na kibali mbele za Mungu.

Pastor Eliya

Comments