Kardinali Pengo ©ipp media |
Akiweka bayana kuhusu maoni ambayo hawakubaliani nayo, Askofu Mkuu wa
Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo,
amesema kuwa masuala ya kuoana mwanaume kwa mwanaume (ikiwemo mwanamke
kwa mwanamke), au kuua wazee, au utoaji wa mimba, basi ni mambo ambayuo
dhahiri hawatakubaliana nayo, ikiwa litakuwa kwenye Rasimu ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Msimamo huu umewekwa bayana pale ambapo Kardinali Pengo alipokuwa
akieleza msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu muundo wa serikali tatu,
tofauti na kama ambavyo vyombo vya habari vilinukuu taarifa kutoka kwa
Tume ya Haki ya Amani ya Baraza la Maaskofu (Katoliki) Tanzania ambapo
walilitaka Bunge kutokashifu mapendekezo ya serikali tatu, kwani
yataleta mshikamano zaidi.
Halikadhalika baraza hilo limesema katika tamko lake hilo kuwa kuna
mambo yenye tija zaidi pia kwenye rasimu hii ya pili, na sio masuala ya
muungano tu.
Kauli ya Mhadhama Kardinali Pengo inatofautiana na ile ya Tume ya Haki
ya Amani ya Baraza la Maaskofu (Katoliki) Tanzania, ambapo ameweka
bayana kuwa huo haukuwa msimamo wa Kanisa Katoliki, na kwamba ingeelezwa
iwapo ingekuwa hivyo.
Rasimu ya kanuni za bunge maalumu la katiba ndio inaendelewa kujadiliwa,
ambayo itatoa mwongozo namna ambavyo mjadala utakuwa na namna ya
kufikia maamuzi kwa vifungu vya rasimu ya pili ya katiba, ambapo baada
ya hapo kura za wananchi (walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la
wapiga kura) ndio watakaoamua.
chanzo : Gospel kitaa
Comments