Kilema atembea baada ya maombezi kwa mtume Peter Rashid Abubakar

Peter Rashid Abubakar
Mama mmoja ambaye amefanya tendo la imani kwa kuchukua hatua ya kwenda kanisani kuombewa na kupokea uponyaji wake aliouhitaji kwa muda mrefu.

Mama huyo ambaye alipata ajali mbaya siku za nyuma na kuwekewa vyuma kwenye miguu  lakini akiwa hawezi kutembea hadi kwa msaada wa magongo leo ametembea baada ya maombezi kutoka kwa mtumishi wa MUNGU Mtume. Peter Rashid Abubakar wa kanisa la GLORY TO GOD MIRACLE CENTER(HOUSE OF PRAYER FOR ALL NATIONS)  Mbezi mwisho jijini Dar es salaam.

YESU yuko kazini na yuko tayari kuwaponya wote walio tayari. Ndugu kama una hitaji lolote kimbilia kanisani na MUNGU atakuponya kupitia maombezi.



                Mama huyu atembea na kuacha magongo chini!
Kwa YESU KRISTO yote yanawezekana.


Mtume. Peter Rashid Abubakar akimuombea mama huyu  ambaye alipelekwa kanisani kwa   usafiri wake binafsi bila kutembea  kutokana na ajali iliyompata na mguu wake akawekewa vyuma lakini baada ya maombi ya Mtume mama huyu akatembea kwa jina la YESU KRISTO.

BAADA YA KUPONA
KANISANI GLORY TO GOD MIRACLE CENTER(HOUSE OF PRAYER FOR ALL NATIONS)

Comments