KUILIMA NA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI * sehemu ya kwanza *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Nasema;
Haleluya...

Blessed be the name of the Lord,
Say;
AMEN.

Kazi yangu kubwa siku ya leo ni kukuwekea msingi wa fundisho hili zuri.Kumbuka leo ni siku ya kwanza ya fundisho,na tunaanza kuweka msingi kupitia kitabu cha MWANZO,Kitabu nikipendacho sana.

Tunasoma;
"Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa.
Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi.hapakuwa na mche wa kondeni bado,wala mboga ya kondeni haijachipuka bado,kwa maana BWANA Mungu haijainyeshea nchi mvua,
wala hapana mtu wa kuilima ardhi;"Mwanzo 4:-5.

Haleluya....

Biblia inaeleza vizuri kabisa sababu ya kutokuwepo kwa mche wa kondeni pamoja na mboga ya kondeni. Biblia inasema sababu ya kwanza ya kutokuwepo mche na mboga ya kondeni ni ;
*Kukosekana kwa mvua.
Mvua ni mojawapo ya sababu iliyoifanya mche na mboga ya kondeni isichipuke.

Kwa lugha nyingine ni kwamba;
Uwepo wa mche na mboga ya kondeni ulitegemea uwepo wa mvua.Uwepo wa mvua ulishikilia maisha ya mche na mboga ya kondeni.Ardhi haikuwa hai kwa sababu BWANA Mungu hakuinyeshea mvua bado.Mboga ya kondeni haikuweza kuchipuka,ikiwa na maana kuwa uhai wa mboga ya kondeni ulikuwa ndani yake,lakini Mvua ilizuia ukuaji.

Haleluya...
Nasema Haleluya....
Naamini Bwana anazidi kukuhudumia saa hii,
Sasa sikia hii tena;

Tazama Biblia inatuambia sababu nyingine kubwa ambayo ni sababu ya pili iliyozuia uwepo wa mche na mboga ya kondeni.
"BWANA Mungu hakuinyeshea nchi mvua,WALA HAPANA MTU WA KUILIMA ARDHI."
Ohoo!
Kumbe!

Kukosekana mtu wa kulima ardhi ni sababu kubwa ya pili iliyozuia mche na mboga ya kondeni kuwepo.Mtu alipokosekana,mche wa kondeni ulikosekana,
mtu alipokosekana,mboga ya kondeni pia ilikosekana.Kwa lugha nyingine ni sawa na kusema,Uwepo wa mche na mboga ya kondeni ulifichwa ndani ya mtu.Kulikuwa hakuna maana ya kuwepo kwa mche na mboga ya kondeni pasipo MTAWALA.

Ohoo!
Kumbe,
MTU ALIKUWA NI MTAWALA!
ALIUMBWA ILI ATAWALE.

Nimegundua sasa kumbe BWANA Mungu hakuruhusu chochote ardhini kimee pasipo ya MTAWALA.Uwepo wa mtu chini ya jua ni kumuabudu BWANA Mungu,pamoja na kumuwakilisha Bwana Mungu kwa kuyafanya mapenzi yake,pamoja na KUTAWALA samaki wa baharini,ndege wa angani,na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.(Mwanzo 1:28)

Hivyo;
Mche na mboga za kondeni zilisubiri uwepo wa mvua kutoka kwa Bwana Mungu,lakini zaidi sana uwepo wa mtu wa kuilima ardhi.Ardhi haikuwa na maisha,uhai;
Mtu alipoumbwa alikusudiwa kuilima na kuitunza ardhi ambayo BWANA Mungu aliifanya.Ardhi ilisubiri ujio wa mtawala,ambaye ni mtu.Hivyo wewe usomaye fundisho hili ujue kuwa mche na mboga za kondeni havikuwa dhahili vilikusubili wewe mtu.

Ukiendelea kidogo kusoma andiko hilo utaona kwamba BWANA Mungu anainyeshea mvua ardhi.
"ukungu ukapanda katika nchi,ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi." Mwanzo 2:6
Hata hivyo tunaona mvua bado haikufua dafu,yaani mvua haikukidhi udhihirisho wa uwepo wa mche wa kondeni,wala mboga ya kondeni.Why?

JIBU;
Sababu ni ile ile ya kukosekana kwa mtu wa kuilima ardhi.

Ndiposa BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,akampulizia puani pumzi ya uhai;mtu akawa nafsi hai (Mwanzo 2:7).Ujio wa mtu aliye hai,ulikamilisha kuchipua kwa mche na mboga ya kondeni. Kwa lugha nyingine;
mtu alibeba roho ya miche na mimea,maana pasipo yeye miche ilikuwa ni ufu.

Mtu ambaye ni nafsi hai,amekuwa kama mbegu ndani ya ardhi.Kumea,kuchipua kulishikiliwa na mtu aliyepewa uhai naye akawa nafsi hai.
Hii ni siri ya ajabu sana ambayo binafsi sijawahi kuisikia ikifundishwa na mtu yeyote yule,hakika ni ya tofauti.

Haleluya...

Tazama sasa mtu ameiendea ardhi iliyokuwa imekufa,alipowekwa tu katika nchi,ardhi ikawa hai,miche ikachipua. BWANA Mungu akaona ni vyema kabisa.

Sasa nakuomba sana unisikilize kwa makini sana hapa;
tunasoma:
" BWANA Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni,akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya."Mwanzo 2:8

Baada ya uwepo wa mvua,kisha BWANA Mungu akamfanya mtu,aliye nafsi hai,tunasoma sasa BWANA Mungu akapanda bustani.
Fahamu kwamba;
kile kilichopandwa ni bustani.
Edeni haikupandwa.

Biblia inasema bustani iliyopandwa,ilipandwa upande wa mashariki wa Edeni.
Kwa lugha nyingine ni kwamba;
Bustani ilikuwa ndani ya Edeni.
Kama ni hivyo basi,ina maana Edeni ilikuwapo kabla ya bustani.
Biblia hajasema Edeni ilipandwa Bali inaeleza kuwa BUSTANI imepandwa ndani ya EDENI.

SASA,
EDENI NI BUSTANI?
AU
EDENI NI NINI?

JIBU;
Nilipokuwa Israeli nikijifunza mambo mbali mbali ya kiimani,sababu asili yetu sisi wakristo imeanzia kule mahali ambapo mitume pamoja na Bwana Yesu ndio asili yao.
Kati ya maswali niliyokuwa nikitafuta kujua ndilo swali hilo,Hivyo;
Nilibahatika kumuuliza tour guide ya kwamba ;

" Where is Eden?"
then,He answered me,;
"Eden is in your heart "

Nikasema ahaaa!
okey,nimeelewa sasa.

Haleluya...
Jina la Bwana Yesu lisifiwe sana...

Kili alichokisema kiongozi wangu wa Israeli,ni kwamba,Edeni ipo ndani yangu.Hivyo;
EDENI NI UWEPO WAKE MUNGU BABA.
Wala,
EDENI sio bustani kama bustani ya kawaida,Bali Eden huwakilisha UWEPO wa kiungu.Biblia inaeleza kuwa Edeni ilikuwapo tu siku na siku,miaka na miaka,Edeni haina mwanzo.

Wengi leo hii hufikiri Edeni ni bistani ya maua hivi,au bustani ya mboga mboga za majani fulani hivi. Hapana !
Jambo hili limefichika hata kulijua.

Sasa tunawezaje kuilima na kuitunza bustani ya Edeni,ikiwa Edeni si bustani kama bustani za kawaida?

UTAENDELEA....

*USIKOSE KABISA MAHARIFA HAYA!

Kwa huduma ya maombi na maombezi,usisite kunipigia simu yangu sababu wakati wenyewe ndio sasa,hata saa ya wokovu wenyewe ndio sasa.Ninachokijua mimi ni kwamba lipo kusudi hata wewe leo kufuatilia fundisho hili,basi nipigie tuombe pamoja juu jambo lolote lile.
piga;
0655-111149

UBARIKIWE.

Comments