KUKOMBOLEWA NA NGUVU ZA KABURI

BWANA YESU asifiwe,
Karibu tujifunze pamoja ujumbe huu muhimu.
pia nakuomba usome hadi mwisho maana ni ufunuo huu utakaokufaa sana, pia shirikisha wengine na kama ni mwalimi wa neno la MUNGU fundisha wengine pia.

Kukombolewa na nguvu za kaburi kunahitajika sana katika maisha yako.MUNGU mwenyezi anasema  ''Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa;- Hosea 4:6a''
- Neno la MUNGU ndio maarifa sahihi ya kuyashika.
-Watu wengi wanajuhudi sana katika mambo mengi lakini sio katika maarifa. 
  ''Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa.-Warumi 10:2''
-Acha kwenda kanisani kutembea tu au kutafuta mchumba bali nenda kanisani kukutana na BWANA YESU. 

Maarifa sahihi ni pamoja na kutambua nguvu za ulimi, na jinsi ambavyo ulimi unaweza kuleta madhara makubwa.

Tambua kwamba ulimi unaumba, na kwa sababu ulimi unaumba je ulimi wako umekuumbia mambo mangapi ambayo yamekutokea? ulimi wa maadui zako umekuumbia mambo mangapi ambayo yamekupata?

Watu wengi huamini kwamba ndimi za wazazi wao tu ndizo zinaumba mambo ambayo huja kuwatokea watoto wao. mfano Mama akimlaani mtoto wake huja kutokea lakini napenda kukuambia kwamba sio ndimi za wazazi tu ndizo zinaumba bali kila ulimi unaweza kuumba jambo kwa mtu yeyote, ila jambo hilo linaweza kutokutokea tu kama mtu huyo ni mtu wa maombi akiwa ampe BWANA YESU maisha yake.

BWANA YESU pekee ndio anaweza kukukomboa na nguvu kaburi inayokukabili.
BWANA anasema
  ''NITAWAKOMBOA NA NGUVU ZA KABURI; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.-Hosea 13:14'' 

Ndugu yangu tunataka juhudi ndoto, mafanikio makubwa maana BWANA YESU alitukomboa  kwa kila kitu.

BWANA ametukomboa na nguvu za kaburi.
-Huduma yako inafuatilia  na nguvu za mauti ili ife kabisa.
-Kazi yako inafuatiliwa na nguvu ya mauti ili ufukuzwe kazi.
-Masomo yako yanafuatiliwa na nguvu za mauti ili ufeli.
-Ndoa yako inafuatiliwa na nguvu za kaburi ili muizike kabisa kwa kuachana.

Mpendwa hata kama unajiona uko salama na ndoa yako ipo salama lakini tambua hii ya kwamba nguvu za kaburi zipo kwa ajili ya kukuangamiza, kuangamiza biashara yako, shetani analeta nguvu za kaburi ili tu kuua kila jambo jema unalotaka kufanya lakini BWANA YESU leo anasema ATAKUKOMBOA NA NGUVU ZA MAUTI zinazotumwa kwako, kwenye ndoa yako , kwenye masomo yako au kwenye Interview unayoifanya.
nenda kanisani kuombewa au kama umeokoka fanya maombi ya nguvu ukimwita BWANA YESU akukomboe.

-Adui yako wa kwanza  ni ulimi wako unaojinenea mabaya kila siku pia ulimi wa wengine unaokunenea mabaya.
  ''Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.-Mithali 18:21''

Ulimi unaweza kuamua maisha yako, na neno hapo juu linasema kuna matunda katika ulimi au katika matamshi na matunda hayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya.

Ndugu yangu anza kuanzia leo kujinenea mazuri, jitabirie baraka tu.
-Kuna mapigo katika ulimi, yawezekana unavyoishi leo ni vile ambavyo ulinenewa zamani,
-Wachawi kila siku wanatoa sadaka na kunyuniza damu za kuku  huku wakitamka ugonjwa fulani ukupate, kama huna maarifa ya neno la MUNGU na sio mtu wa maombi hakika jambo hilo litakupata.
Ulimi ni hatari sana.
-Siku chache zilizopita ROHO MTAKATIFU aliniambia kwamba nifute maneno yote mabaya niliyotamkiwa na watu haijarishi ni watumishi wa MUNGU au mtu yeyote lakini kama aliwahi kuninenea jambo baya ina maana jambo hilo bado lipo linanifuatilia hivyo nifute maneno yote mabaya niliyowahi kutamkiwa na pia kwa sasa ni utaratibu wangu kufuta maneno yote mabaya ninayonenewa.
Ndugu ufunuo huu husika nao pia na wewe, futa kila neno baya ulilonenewa na mtu yeyote hata kama ni wazazi, futa kwa jina la YESU KRISTO.
Neno la MUNGU linasema  '' Utafichwa na mapigo ya ulimi; Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.-Ayubu 5:21''
Hapo tunajifunza kwamba kumbe kuna mapigo ya ulimi lakini pia kumbe yupo MUNGU atakayetushindia. Lakini MUNGU atatushindia tu kama tuko upande wake.

Ashukuriwe BWANA YESU aliyekuja kutupa uzima kisha uzima tele, yaani alikuja kutupa uzima sana na kisha uzima wa milele.(Yohana 10:10b)

Mtumishi wa MUNGU anasema  ''Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya, Atakufa lini, jina lake likapotea?-Zaburi 41:5''

Hata wewe ndugu wapo wengi wanaokuzika huku ukiwa hai, 
wapo wanaokunenea mabaya ya kukua kila siku, 
wapo wanaokuendea kwa waganga ili tu ufe au usifanikiwe, 
wapo wanaotamani ufe ili washangilie kisa tu wewe ni mtumishi wa MUNGU. 
Wapo wanaotamani ufe ili wachukue nafasi yako kazini maana wewe ni mkuu wao wa kazi. Hizo zote ni nguvu za kaburi, mkimbilie BWANA YESU leo ili uwe salama. umeijua siri hii mkimbilie BWANA YESU leo na utakaa salama.


''Amemeza mauti hata milele; na BWANA MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.-Isaya 25:8''

Ni ahadi nzuri sana ya MUNGU kwako.
Hata kama wachawi waliomeza mauti wataitemea kazini kwako au kwenye afya yako lakini ukienenda katika BWANA YESU utakaa salama, maana kama watakunenea mabaya kwa miezi 7 lakini unauwezo wa kuyafuta maneno yao kwa dakika 1 tu kwa maombi kupitia jina kuu la YESU KRISTO.

 -Wapo wameshajimbiwa makaburi wangali wako hai,
-Wapo watu wameshatengenezewa majeneza wangali wakiwa hai.

Ona hapa, siku BWANA YESU anakufa bale msalabani, kuna matukio makubwa yalifanyika na hapa tunaona hata nguvu ya kaburi kuwa haina kazi tena kwetu tutakaompokea kama BWANA na MWOKOZI wa maisha yetu. Hapa makaburi yalifumka na watakatifu wakafufuka, ndugu yangu BWANA alitangaza ushindi kwako, Hutakufa bali utaishi ili uyasimulie matendo makuu ya MUNGU katika maisha yako.
''Naye YESU akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.-Mathayo 27:50-53''


Kwa YESU KRISTO tunashinda na zaidi ya kushinda.
Usiacha kufuatilia hapa mafundisho na habari za kikristo hapa Maisha ya ushindi.
 na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.

                        MUNGU akubariki sana .

                         Ni mimi ndugu yako

                           Peter M Mabula

                   Maisha ya Ushindi Ministry.

Comments