KUPENDA KUUTUMIKIA ULIMWENGU NA WANADAMU:

Watu Wengi wako tayari kuutumikia ulimwengu na wanadamu kwa gharama yoyote na wanaona ni karaha kumtumikia Mungu aliye hai. Wengine wanakuwa tayari kutumika kwa bidii zote kama Yakobo alivyomtumikia Labani miaka saba kumpata Raheli na akaona miaka saba ni siku chache sana kwa vile alivyompenda Raheli [MWANZO 29:18-20].

Vivyo hivyo watu wengi wakati wa Biblia walitoa mioyo yao yote kumtumikia Farao na Kaisari [1 SAMWELI 2:27]; [YOHANA 19:12], Kedorlaoma [MWANZO 14:4] n.k.

Vivyo hivyo leo, watu wengi wameweka mioyo yao yote katika kuutumikia ulimwengu huu katika ofisi za serikali, mashirika na kampuni mbalimbali, na kazi mbalimbali za dunia hii, kama katika kilimo, ufugaji, biashara n.k Vivyo hivyo leo, watu wengi wameweka mioyo yao yote katika kuutumikia ulimwengu huu katika ofisi za serikali, mashirika na kampuni mbali mbali na kazi mbalimbali za dunia hii katika kilimo, ufugaji, biashara n.k. Kazi hizi zote ni njema. Biblia inasema kwamba asiyefanya kazi na asile [2 WATHESALONIKE 3:10. 

Hata hivyo thawabu ya utumishi wote tulio nao kwa ulimwengu ni ujira tuu tunaopata ambao mwisho wake ni hapahapa duniani. Utumishi wetu kwa ulimwengu huu ni kujiwekea hazina zetu duniani, na hazina yetu ilipo, ndipo na mioyo yetu itakapokuwepo [MATHAYO 6:19-21]. 

Ikiwa tunahitaji thawabu zinazodumu, basi, pamoja na kufanya utumishi wa ulimwengu huu, ni huhimu kutenga muda wa kutosha katika kumtumikia Mungu. 

SHIME NDUGU ZANGU TUITENDE KAZI YA BWANA.

MUNGU akubariki sana
By  Erick Mkinga

Comments