MAMBO MUHIMU KUHUSU JINA LA YESU (Sehemu ya kwanza).


Bwana Yesu asifiwe sana,
Nickson Mabena

 tunamshukuru Mungu kwa kutupa nafasi nyingine ya kushirikishana maneno ya uzima... Kuna msemo unasema, "SIRI YA KUFUNDISHA NI KUFUNDISHWA",
Na Biblia inasema , "IMANI CHANZO CHAKE NI KUSIKIA"... 

Niliwahi kujifunza mahali somo hili, nmeona nikushirikishe na wewe, ili tubarikiwe pamoja!!

1.Hakuna wokovu katika mwingine.

"Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo". Mdo 4:12a 


"Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao." Mathayo 1:21


"Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;" Yoh 1:12


"kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka". Rumi 10:13
 
maandiko hayo yanatuthibitishia kwamba, JINA LA YESU ndilo JINA pekee linalookoa!!.



2.Ni amri kuliamini Jina la Yesu Kristo (SIO OMBI)

"Na hii ndiyo AMRI yake, kwamba TULIAMINI JINA la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri" 1YOH 3:23


"Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu." Yoh 3:18

Hii inashangaza sana, kumbe ni Amri kuliamini JINA la YESU na wala sio Jina la Kanisa, au jina la Dhehebu, au Jina la Mtume wala Nabii yeyote!!.

3.Kuna uponyaji katika Jina la Yesu.

"Na Ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa Jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakita wadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Marko 16:17-18


"Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliitia jina la BWANA ataponywa;......." Yoeli 2:32a

Kwenye JINA LA YESU, pia kuna uponyaji!!.
Jina la Yesu ni jina la Ajabu sana duniani kuliko majina Yote; Endelea kulifatilia somo hili,naamini kuna kitu Roho Mtakatifu atakuongezea, kwenye moyo wako.
Mtu aliyetafakari vizuri juu ya Jina hili lenye uweza wa Ajabu, basi hawezi kabisa akawa anahubiri DHEHEBU, KANISA au kitu kingiene chochote!!.

UBARIKIWE KWA KUUSOMA UJUMBE HUU!.
...........LITAENDELEA>>>>>>>>>


                                By Nickson Mabena

Comments