MAMBO MUHIMU KUHUSU JINA LA YESU (Sehemu ya pili)


Bwana Yesu asifiwe sana, 

tunamshukuru Mungu ametupa neema nyingine tena ya kuendelea kujifunza maneno yake ya uzima...

Tunaendelea na somo letu tulilolianza wiki iliyopita, lakini leo ni sehemu ya pili, kama ulikosa sehemu ya kwanza ya somo hili basi hujachelewa, waweza kulitafuta kwenye page yetu ya Utukufu
Kwa MUNGU.


Ngoja tuendelee kuyaangalia haya mambo muhimi kabisa ambayo mtu anatakiwa kuyatafakari kwa kina kuhusu Jina la Yesu.

4.Lolote ulifanyalo-lifanyike kataka Jina la Yesu.
 
"Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye"
Kolosai 3:17


5.Kuomba na Kupewa katika Jina la Yesu Kristo.
 
"Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa Jina langu, nitalifanya." Yoh 14:13-14


Mambo mengine kama hayaingii akilini vile, eti tuombe kupitia Jina...

Hili jina ni la ajabu sana, ukitumia mda kulitafakari hili jina Roho Mtakatifu atakufunulia vitu vingi sana kwenye roho yako.


"Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa Jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu". Yohana 16:23-24

kila mtu anatamani sana maombi yake yajibiwe, lakini Yesu anatufundisha kwamba, ili furaha yetu iwe timilifu ni lazima tuombe kwa Jina la Yesu.

6.Jina lipitalo kila jina.
 
"Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa Jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba." Filip 2:9-11


Hii ndiyo funga kazi, yaani Jina la Yesu linapita kila Jina...
Kila goti litapigwa kwa jina la Yesu, ingawa kuna watu wanajitahidi ili majina yao yawe juu, lakini Jina la Yesu ni mwisho wao.
Mungu akubariki sana kwa kulifuatilia somo hili, Ombi langu kwako ni kwamba endelea kumtumaini Yasu, kwani bado anaweza... Usiache kuomba!!


Pia kama hujampokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa Maisha yako yaani HUJAOKOKA na ungependa kufanya hivyo , hujachelewa bado waweza kuwatafuta watumishi wa Mungu wakusaidie kwa hilo... Pia unaweza kunitafuta hapahapa, ili tuangalie liwezekanalo.

Mungu akubariki sana kwa JINA LA YESU!!.
By  Nickson Mabena

<<<<Amen, Amen>>>>

Comments