BWANA YESU
KRISTO apewe sifa ndugu zangu.
Ni siku
nyingine nzuri aliyoifanya BWANA, ambapo tunakutana hapa ili tujifunze neno la
MUNGU.
Namshukuru
sana MUNGU kwa kunipa ujumbe huu mzuri wa kulifaa kanisa lake kokote duniani.
Karibu.
Maneno
hutoka katika kinywa.
Kinywa
kinaumba.
Unaweza
ukamtamkia mtu jambo likawa, haijalishi ni jambo jema au baya.
Kikwazo
kikuuu cha kuwakwamisha watu wa MUNGU ni kinywa. (Mithali 18:20-21 ''Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake).
-Kuna
mamlaka katika kinywa chako mtumishi wa MUNGU.
-Kuna
mamlaka katika kinywa chako wewe uliyempa BWANA YESU maisha yako.
Uwe makni
sana na hakikisha kinywa chako kina mema na sio mabaya.
-Kama
watumishi wa KRISTO, tukitamka mabaya tujue tunamrudisha YESU KRISTO msalabani.
Haijalishi
haya unayatamka kanisani au nyumbani, njiani au kazini.
-Hakuna haja
ya kuwa watakatifu kanisani tu, bali tuwe watakatifu na nyumbani pia.
‘’Kinywa
changu lazima kitamke mema kwa watu wa MUNGU’’
-Ukikiri
uzima utapokea uzima na ukikiri mauti utapokea mauti.
Kiri uzima
siku zote za maisha yako.
-Chunga sana
mamlaka iliyo katika ulimi wako.
MUNGU
amekuwa na mawazo mazuri sana juu yetu, lakini sisi siku zote tunakiri ubaya
tu.(Mithali 29:11)
MUNGU hapa
anatutamkia mazuri , kwanini sisi kujitamkia mabaya?
‘’MUNGU ana
makusudi ya kunibariki’’
Tamka baraka
ndugu.
Inawezekana
unakabiliwa na mambo magumu katika maisha, lakini kiri ushindi ukisema ‘’sasa
naenda kushinda’’ kiri ushindi ukisema sasa naenda kuishi maisha ya ushindi kwa
jina la YESU KRISTO.
-Ishi kwa
kutamka mazuri tu.
Lazima uishi
ndani ya YESU na ukiri ushindi ukiwa
ndani ya YESU.
-Siku zote
jifunze kukiri kushinda.
-Enenda kwa
imani huku ukikiri ushindi siku zote.
Omba kwa
imani na wewe unayeombewa pokea kwa imani.
Imani sio
kuona bali imani ni kutarajia na baadae kitu hicho kinakuwa.
''Mathayo
12:36-37-Basi, nawaambia, Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.
Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.''
-Lazima
nitamke vizuri ili hesabu yangu iwe nzuri siku ya mwisho..
-Ndugu yangu
linda sana maneno ya kinywa chako maana kila unavyotamkia wengine ndivyo hivyo
itakavyokuwa na kwako, pia utatoa hesabu
siku ya mwisho.
Kama maneno
ya Daktari yanaweza kumlegeza mgonjwa vipi maneno ya mtu wa MUNGU? Ni zaidi
kuliko ya daktari.
-Jifunze
kutamka mema tu kwa watu na kwa nafsi yako pia.
''Yakobo
3:9-12-Kwa huo(ulimi) twamhimidi MUNGU Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa MUNGU. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haifai mambo hayo kuwa hivyo.
Je! Chemchemi katika jicho moja hutoa maji matamu na maji machungu?
Ndugu zangu, Je! Mtini
waweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Kadhalika chemchemi haiwezi
kutoa maji ya chumvi na maji matamu.''
Uwe makini sana na kila neno unalotamka au unalotamkia watu.
MUNGU
akubariki sana na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi
ndugu yako
Peter M
Mabula
Maisha ya
Ushindi Ministry.
0714252292
Comments