MAOMBI NI SILAHA.



Bwana YESU apewe sifa,
Wakristo wengi wamekua na kawaida ya kutumia biblia(kitabu cha maandiko matakatifu)kama silaha wakiwa safarini,wakienda kulala kama kinga au silaha dhidi ya mashambulizi ya ibilisi.

Ndugu mpendwa,kutumia biblia na msalaba bila NENO(YESU)haiwezi kusaidia kitu. Kumbuka,hata shetani alimjaribu YESU kwakutumia maandiko!
Nakushauri,upende kusoma sana,ili uwe na akiba yakutosha moyoni mwako. Shetani,hushindwa kwa hoja,hata YESU alimshinda kwa NENO hilo hilo alilotumia kumjaribu.

Ukitaka kumshinda shetani,sharti uwe na hamu ya kuomba na kusoma neno kwa wingi. Jione mwenye uhitaji katika masuala ya kuomba,tia bidii katika kujifunza kuomba,tamani kujua zaidi namna ya kuomba{LUKA 11:1}

Ndugu mpendwa,hakuna anaeweza kusimama nje ya maombi,tunajifunza kwa manabii wa kale hata YESU mwenyewe,walidumu katika maombi na imani juu ya MUNGU.


"MUNGU AKUBARIKI SANA"



Mungu akubariki na kukuinua, akufunulie zaidi na zaidi umjue sana na kumpenda, Katika Jina la Yesu Kristo nimeomba.
Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


sos.sesi@yahoo.com.
Simu +255 712 909 021.
+255 784/757 464 141.

Comments