MAONO NA NDOTO * sehemu ya mwisho *


Na Mtumishi Gasper Madumla
Nakusalimu mpendwa katika jina la BWANA YESU;
Bwana Yesu asifiwe...
I say to you,blessed be the name of Jesus...
say;

Amen...
Leo tanakwenda kumalizia sehemu ya mwisho pia siku ya leo ni siku ya tisa ya fundisho hii ambapo,tunaenda kujifunza tena kwa sehemu yake kwa habari ya ndoto.
Kumbuka msingi wa fundisho hili unatoka katika kitabu cha Matendo 2:17.

NDOTO.
Wapo watu chini ya jua hili huitwa ''waota ndoto".Watu wa namna hii wamepewa kuona mambo fulani katika ndoto.

Mfano;
Mtu mmoja alinijia na kuniambia; " ...mtumishi niliota ndoto,nikaona watu kama majambazi wameingia nyumbani kwangu na kuanza kuiba,...kisha nilipoamka asubuhi baada ya ile ndoto,yaani ile natoka nje tu,gafla nikakutana na umati wa majirani zangu ambao wengine walikuwa wakilia kwa ajili yangu.
Maana walidhani nimeuwawa usiku ule sababu kulikuwa na majambazi kweli ambao waliingia ndani ya chumba changu cha kulala wakiwa na silaha na nondo kadhaa mikononi mwao.
Khaa!
Kumbe kile nilichokuwa nakiota usiku kumbe ilikuwa ni tukio halisi lililokuwa likiendelea huku mimi naota tukio hilo hilo.

Majirani zangu wakaanza kunishangaa kwamba mimi ni mzima lakini nilipoingia ndani nikagundua waliniibia baadhi ya vitu vyangu vya thamani....
lakini tazama mtumishi,kile nilichokuwa nakiota ndicho kilikuwa kinafanyika muda ule ule..."
Hayo yalikuwa ni maneno ya mpendwa mmoja aliyekuwa akinisimulia.
Haleluya....
Jina la Bwana libarikiwe...

Hivyo wapo watu wenye uwezo wa kuona tukio lenye kutukia wakiwa ndotoni.
Nami nakuambia usiipuzie ndoto uotazo.
Siku ya leo tutajifunza fundisho hili kupitia ndoto moja ndogo lakini ndio ndoto ngumu iliyopata kuandikwa katika Biblia.
Ndani ya Biblia tuisomayo kila siku,zipo ndoto mbali mbali,Lakini ipo ndoto moja yenye kuonekana ndogo lakini ndio ndoto ngumu kuliko zote.
Tunasoma:

"Hata katika mwaka wa pili wa Kumiliki kwake Nebukadreza,Nebukadreza aliota ndoto;na roho yake ikafadhaika,usingizi wake ukamwacha.
Ndipo mfalme akatoa amri kuwaita waganga,na wachawi,na wasihiri na Wakaldayo,wapate kumweleza mfalme ndoto zake.Basi wakaingia,wakasimama mbele ya mfalme.
Mfalme akajibu,akawaambia Wakaldayo,Neno lenyewe limeniondoka;msiponijulisha ile ndoto na tafsiri yake,mtakatwa vipande na nyumba zenu zitafanywa jaa." Danieli 2:1-2 & 5
Biblia imeeleza kuwa Nebukadreza,alipoota ndoto ile,usingizi wake ulimwacha kwa lugha nyingine hakupata usingizi kwa sababu roho yake ilifadhaika.
Alichokihitaji Nebukadreza ni kupata tafsiri sahihi ya ndoto yake pasipo kudanganywa.Yeye mwenyewe hakuwa na uwezo wa kufasiri hiyo ndoto,Ndiposa akawaita wachawi,waganga,wasihiri,na Wakaldayo.
Haleluya..
Wachawi,waganga na wasihiri walikuwa na mtihani mkubwa sana sababu uwepo wa maisha yao ulitegemea kuweza kutafsiri ndoto kwa usahihi,la sivyo maisha yao yapo hatarini.Hata hivyo hawakuweza kutafsiri ndoto ya mfalme.
Ndoto hii imekuwa ni ndoto ngumu kutafsiriwa sababu kile kilichokuwa kimeotwa kimesahaulika,Nebukadreza anasema;
"...Neno lenyewe limeniondoka;.." Danieli 2:5
Waganga na wachawi walitegemea labda watapewa chanzo cha ndoto hiyo ili wao waanzie hapo kutafsiri,lakini hali haikuwa hiyo.
Walitakiwa watafsiri ndoto ambayo haina chanzo chochote kile.Hii ilikuwa ni kazi kubwa kuliko maelezo,Hivyo hakuna aliyeweza kutafsiri ile ndoto,si wachawi,wala waganga,wala wabashiri,wala Wakaldayo.

Ndiposa wakamtafuta Danieli na wenzake ili wauwawe (Danieli 2:13) Maana walijua hata wakina Danieli na wenzake hawataweza kutoa majibu ya ile ndoto,sababu yeye aliyeiota kwanza haikumbiki lakini cha ajabu yeye aliyeota anahitaji majibu.
Haleluya...
Jambo moja la mdingi tunalojifunza siku ya leo ndilo hili;
*Hakuna hawezaye kufasiri ndoto asipoongozwa na Mungu.
Tunasoma;
" Ndipo Danieli akaenda nyumbani kwake,akawapasha habari kina Hanania,na Mishaeli,na Azaria wenzake;
ili waombe rehema kwa Mungu wa mbinguni kwa habari ya siri hiyo,ili kwamba Danieli na wenzake wasiangamizwe pamoja na wenye hekima wa Babeli." Danieli 2:17-18

Jina la Bwana litukuzwe...
Nampenda Danieli tazama;
Danieli alipoitwa mbele ya mfalme hakuwa na haraka kusema,maana alijaa hekima za tofauti kabisa,naye Danieli alitambua jambo moja kwamba hata yeye mwenyewe hana uwezo wa kutafsiri ndoto ile,na akajua ya kwamba ni Mungu tu ndiye mwenye kutafsiri ndoto zote kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Danieli akapiga hesabu kubwa kisha akajua ahaa!
lazima amfuate Mungu aliye hai,Mungu wa utaratibu.

Ndiposa,Danieli akaenda kuwapasha habari rafiki zake.
Sasa unisikilize;
Upatapo jambo kubwa kama hilo yakupasa kuwaendea rafiki zako wa kiroho ambao mtaambatana kiroho.Wapo marafiki wasioambatana kiroho yaani marafiki wasiokuwa na roho moja na wewe.

Danieli aligundua hili,ndiposa akawaendea rafiki zake wenye roho moja. Ninaposema watu wenye roho moja nina maanisha watu walio tayari kubeba mzigo wako,pale unapokuwa na shida,basi shida hiyo nayo ni ya kwao,raha zako ni raha zao.
Kile utakachokiomba ndicho hicho hicho watakachokiomba.Watu wa namna hii ni watu wenye muambatano wa robo moja.
Haleluya...
Wakina Danieli wakaenda kumuuliza Bwana Mungu kwa habari ya kupewa majibu sahihi ya ndoto ya mfalme,naye Bwana akawajibu.
Oooh,Haleluya..

kile walichokishinda wanadamu,Mungu ameshinda.Mungu amefanya njia pasipo na njia.
Hivyo ifike wakati ambapo tusitumie akili zetu kupambanua ndoto,ni lazima.Pia tupatapo jambo lolote gumu,yatupasa kuwashilikisha wenzetu watu wa rohoni ili tuungane pamoja kuomba mbele za Mungu.
Wengi tunapata NDOTO katika nyakati hizi za mwisho,lakini swali la kujiuliza ;
Je tunazifanyia kazi ndoto tuotazo?

Ikiwa umeota ndoto,yakupasa kumuliza Mungu kwanza kabla ya mwanadamu yeyote yule.Hata baadaye ndipo waweza kumuuliza mtumishi wa Mungu.
Mungu huendelea kusema nasi kwa njia tofauti tofauti kabisa mfano aweza sema nasi kwa njia ya UNABII, MAONO na NDOTO (Mate do 2:17) kama tulivyojifunza.
MWISHO.
Najua utakuwa umebarikiwa sana kama wengine walionipigia simu jinsi walivyobarikiwa. Kumbuka jambo moja;
SAA YA WOKOVU NI SASA,
piga namba yangu hii,na Bwana atakuhudumia;
0655-111149

UBARIKIWE.

Comments