MAONO NA NDOTO * sehemu ya nne *

Na Mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu apewe sifa...
Nakusalimu mpendwa katika jina la Bwana,nikisema;
Haleluya...

Leo ni siku ya nne ya fundisho hili mahali hapa.Wengi waliokuwa wakifuatilia fundisho hili kwa njia ya mtandao wanasema;
wamebarikiwa sana na wamepokea mafunuo mengi kupitia fundisho hili.

Kumbuka;
Tulikuwa tukijifunza namna ya maono yanavyoweza kukamilishwa.Tukaangalia njia mbili ambazo MAONO hukamilika,njia hizo ni njia ambazo maono yanaweza kupitia,nazo ni;

a)Maono kwa njia ya macho ya wazi wazi.
b)Maono kwa njia ya usingizi./Kuzimia kwa roho.
(Fuatilia sehemu zilizopita,ili uelewe vizuri mahali tulipotoka)

Haleluya...
Sasa tunaendelea;

Biblia inasema;

" Nalikuwa katika Roho,siku ya Bwana;nikasikia sauti kuu nyuma yangu,kama sauti ya baragumu," Yohana 1:10

Katika andiko hilo,tunaposoma ya kwamba "nikasikia.....sauti kama ya baragumu"
lile neno " nikasikia..."
lina maanisha kwamba,
masikio ya rohoni ndio yalisikia ile sauti iliyo kama ya baragumu kwa sababu Yohana alikuwa katika roho.

Kwa lugha nyingine Yohana hakusikia ile sauti kwa masikio yake ya damu na nyama,Bali alisikia kwa masikio ya rohoni. Hivyo basi ikiwa Yohana alipata kusikia sauti pindi alipokuwa rohoni,basi;inaonesha yapo masikio ya rohoni yenye kusikia sauti ya BWANA MUNGU.

Yohana ilipokuwa akiyapata maono hayo alikuwa kama mtu aliyekufa (Yohana 1:17). Ndio maana maono haya hujulikana kama maono kwa njia ya usingizi.

Haleluya...

Sasa unisikilize tena;
Tumeaona watu waliopata maono makubwa kama akina Yohana,Musa,akina Ezekieli,pamoja na Samueli,pamoja na Petro,pamoja na Kornelio,N.K ;
hao wote wakiwa wamepata maono kwa njia ya usingizi/kuzimia kwa roho au kwa njia ya macho ya wazi wazi kama tulivyojifunza hapo awali.

Watu hao waliopata maono,walikuwa ni watu wa rohoni. Watu wenye kubeba kusudi la Mungu. Nasi leo hii tukitaka kuwa na MAONO makubwa kama hayo ni lazima tuwe watu wa rohoni kweli kweli.

Mungu huzungumza nasi kwa njia nyingi,na kwa njia tofauti tofauti; miongoni mwa njia hizo ni njia ya MAONO.Shida moja tuliyokuwa nayo leo ni kukosa MAONO. Ikiwa tunakosa maono,

Basi ipo shida ndani yetu.
Si kana kwamba Mungu hasemi nasi siku za leo,Au
Si kana kwamba Mungu hakuachilia nguvu ya maono kwa watu wake,Bali maono yamekwisha achiliwa (Matendo 1:17) lakini shida tuliyonayo sisi ni MIKAO yetu tuliyokaa ndani ya maisha ya ukristo,mikao yetu hayampendezi BWANA MUNGU.

Sasa,
Ikiwa kama tunataka kuwa na maono makubwa kama waliyoyaona watu wa Mungu wa kipindi kile,basi ni lazima tubadili mikao yetu mbele za BWANA MUNGU.Mikao yetu ya kubadili ni kukubali kutoka rohoni kuishi maisha ya utakatifu na kuzichukia dhambi zote.

Sikia;

Watumishi wa Mungu wa kipindi kile walikuwa hawafanyi jambo lolote pasipo kuoneshwa katika MAONO. Watumishi wa Mungu walihitaji kupewa ufafanuzi na maelekezo juu ya kazi waliyoitiwa,mfano;
Musa alipopata maono ( Kutoka 3:1-3) pale alipotumwa aende kwa Farao.

Musa alihitaji kujua maelezo sahihi,namna ya kuanza na kumaliza kazi aliyopewa na BWANA MUNGU,ndio maana Mungu anaanza kumuelekeza ya kwamba yeye ni Mungu wa namna gani aliyemtokea,anaanza kumwambia ya kwambaYeye Mungu anaitwa nani/jina lake Mungu ni lipi,kisha anamtuma.

Hayo yalikuwa maelezo muhimu sana kwa Musa.Pia watu wa Mungu walikuwa wakihitaji kuona MAONO juu ya kazi yoyote ile waliyopewa na Bwana Mungu.
Walikuwa hawaendi kuifanya kazi ya Mungu kwa shauli lao.

Leo,watumishi wamekosa MAONO,Bwana Mungu hakujifunua kwao,kwa sababu ya maisha yao ya dhambi,na wengi huenda kwa kutumia akili zao,na ndio maana huduma inakuwa ngumu sana sababu MAONO hakuna.

Bwana Yesu asifiwe...

Ni maombi yangu,ya kwamba Mungu akaturehemu sisi watumishi wa Mungu wa Tanzania ili tuweze kupata MAONO juu ya huduma tuzifanyazo.

Haleluya...

Nasema;
Maono tuliyojifunza,ni maono kama ishara ya picha. Tafsiri hiyo ya maono kama ishara ya picha ni moja ya tafsiri kubwa sana ambayo waandishi hata walimu wengi hawaielezei kiundani kama sisi tulivyojifunza takribani siku nne mfululizo.

Sasa ;
Imefika wakati wa kukupa tafsiri nyingine ya Maono. Ninaomba uwe makini kabisa kunifuta,ili uelewe vizuri.

Naanza hivi;

Kila mwanadamu aliyeumbwa,aliumbwa kwa maana na kusudi kamili la BWANA MUNGU mwenyewe. Mwanadamu hakuumbwa kwa hasara. Ndio maana Mungu alipomuumba mwanadamu na vitu vingine akaona ya kuwa ni vjema. (Mwanzo 1:31)

Na ikumbukwe ya kwamba, Mungu alihakikisha anamuwekea mwanadamu kila kitu tayari ili mwanadamu aje afanye kazi ya kuvitawala vile vilivyoumbwa...

ITAENDELEA....

Nakuomba sana usikose kabisa fundisho lijalo. Maana lipo neno litakalo kusaidia sana tunapoendelea kujifunza juu ya MAONO na NDOTO.Hapa tulipoishia,bado sijakuelezea kiundani juu ya tafsiri ya hii ya pili ya neno MAONO kwa mujibu wa biblia. Yashike sana hayo,ili tukiendelea tuwe pamoja.

• Kwa huduma ya maombi na maombezi,piga namba hii;

0655-111149.

Comments