MAONO NA NDOTO * sehemu ya saba *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Haleluya....
Nakusalimu nikikuambia;
Bwana Yesu asifiwe sana...

Leo tunaingia katika kipengele kipya kabisa kuhusu NDOTO.Maana katika siku sita zote tulikuwa tukijifunza kuhusu maono.

Wengi wametafsiri neno NDOTO kwa tafsiri tofauti tofauti,ingawa tafsiri nyingine si tafsiri sahihi. Leo tanajifunza tafsiri sahihi iliyo rahisi kabisa ya neno NDOTO.

Ndoto ni nini?
*Ndoto ni mtiririko wa picha zitembeazo katika akili ya mtu,pindi mtu huyo anapokuwa amelala.

Ndoto huja pale mtu anapokuwa amelala,na ndio maana huwezi kumkuta mtu ambaye ajalala,mtu atembeaye kisha akuambie ya kwamba alikuwa anaota ndoto wakati anatembea.

Hakika ukikutana na mtu kama huyo ni lazima utamshangaa !..
Na swali la kwanza utakalo muuliza mtu huyo ni hili;
"Je wakati unatembea ulikuwa umelala,hata uote?"

Na swali la namna hiyo ni swali la msingi kabisa,maana sote twajua kwamba; ili mtu aote inampasa alale.

Haleluya...
Groly to God....

Tofauti ya MAONO na NDOTO.
*Maono yanaweza kuonekana hata pasipo kulala,lakini NDOTO ni lazima muhusika alale ndipo aote

* Maono huusika na roho,wakati NDOTO huusika na akili.
Kumbuka;
Mtu anapolala roho yake i macho,roho ya mtu aliye hai ailali,hivyo mtu anaweza kupata maono akiwa hajalala au hata akiwa amelala(Kama tulivyojifunza siku sita za fundisho hili)
Lakini mtu hawezi kupata ndoto akiwa hajalala sababu ndoto husubiri kupumzika kwa akili.

*Maono huwa na maana na mafunuo ya msingi,NDOTO nyingi huwa hazina maana.
Ndiposa Mhubiri anasema;
" Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi;..."Mhubiri 5:3

>Wengi huota kwa sababu ya miangaiko ya mchana kutwa,wakilala tu pale akili inapopumzika,nao huota. Ndoto za namna hii huwa hazina maana.

*Watu wengi huota ndoto,wachahe sana huona maono.
>Hapa sasa;
Ninajua hata wewe utakuwa umeshawahi kuota ndoto nyingi sana,hata nyingine huzikumbuki hivi sasa,lakini vipi kuhusu maono? UMESHAWAHI KUPATA MAONO YOYOTE?

Leo hii wakitokea watu wawili kisha mmoja aanze kusema hivi;

"...Jana nilikutana na Mungu,akanionesha mambo makubwa kisha Mungu akaniambia..."

Huyu mtu wa kwanza,hawezi kuaminika kiurahisi kwa ushuhuda wake wa kuonana na nguvu za Mungu maana watu watamshangaa ! wakihoji kwamba inawezekanaje akutane na Mungu?

Haya;

Mtu wa pili naye aje na kusema hivi;
"...Jana nilikutana na shetani na mapepo yake...."

Watu wa leo watamuamini zaidi,na kumsikiliza huyu wa pili kwa sababu eti amekutana na shetani na mapepo yake.Ushuhuda wa mtu wa pili umepewa nafasi zaidi ya ushuhuda wa mtu wa kwanza aliyeshuhudia amekutana na Mungu/Nguvu za Mungu katika maono.

Bwana Yesu asifiwe sana...

Mimi siwashangai sana watu wa namna hiyo, wale wenye kukataa kumuamini mtu yule wa kwanza aliyesema ameonana na Mungu sababu kupata MAONO juu ya nguvu za Mungu sio rahisi hata kidogo,tofauti na kuonana na shetani na mapepo yake.

Ndio maana ninakuambia MAONO hupatikana kwa nadra sana,MAONO makubwa ni kwa wale watu wa rohoni,Bali NDOTO ni kwa watu wote.

Haleluya...

Ndoto ni njia mojawapo ya mawasiliano ya ki-Mungu au hata ya kipepo pia.
Nasema ni mawasiliano ya ki-Mungu kwa maana tumeona Mungu akisema na watu wake wengi katika ndoto,akiwaonya,akiwapa maelekezo,au akisema nao juu ya mambo yajayo.

Tazama hapa;
" Na hao walipokwisha kwenda zao,tazama,malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto akasema,Ondoka,umchukue mtoto na mama yake,ukimbilie Misri,ukae huko hata nikuambie;kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize." Mathayo 2:13.

Bwana Mungu anamfikishia taharifa Yusufu kwa njia ya malaika,akimueleza mabaya yanayotarajiwa kufanywa na Herode.
Ndoto ikawa kama chombo cha kukamilisha taharifa ya Mungu kwa Yusufu.Vivyo hivyo Mungu anaeweza kusema nawe kwa njia ya malaika juu ya mambo ya hatari ndani ya maisha yako.

Biblia inaweka wazi ya kwamba Bwana Mungu hujifunua katika maono,lakini husema nasi katika ndoto;

" Kisha akawaambia,
Sikilizeni basi maneno yangu;
Akiwapo nabii kati yenu,
Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,
Nitasema naye katika ndoto."Hesabu 12:6

Haleluya...

Katika nyakati hizi za mwisho,Bwana bado husema nasi katika ndoto,akitufunulia mambo yajayo....

ITAENDELEA...

*Usikose kabisa sehemu ijayo mahali hapa hapa.Na ikiwa bado hujaokoka na unapenda kukata shauri siku ya leo,Basi piga namba yangu hii hapa chini;
0655-111149

*Pia kwa huduma ya Maombi na maombezi,piga namba hiyo hiyo hapo juu.

UBARIKIWE.

Comments