MAONO NA NDOTO * sehemu ya tatu *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe...
Jina lake BWANA MUNGU na lihimidiwe na kila mwenye pumzi na aseme;
AMINA...

Karibu katika sehemu ya tatu ya fundisho hili zuri sana.
Leo tunaendelea tena;

Kumbuka;
Nazungumzia MAONO

Fundisho lililopita tulijifunza kwamba maono yanaweza kukamilishwa kupitia njia mbili. Au kwa lugha nyingine ni kwamba ;
Mtu anaweza kupata MAONO kupitia njia kuu mbili nazo ni;

* Maono kwa njia ya macho ya wazi wazi.
*Maono kwa njia ya usingizi/kuzimia kwa roho.

fundisho lilopita tuliangalia kidogo katika sehemu ya maono kwa njia ya macho ya wazi wazi ikiwa ni njia mojawapo ya kukamilisha maono.Leo tunamuangalia mtu mwingine aliyepata maono kwa njia isiyo ya usingizi./Maono kwa njia ya macho ya wazi wazi.

Mfano mmojawapo mwingine wa mtu aliyepata maono kwa njia ya macho ya wazi wazi ni ; Musa.

Tunasoma;

"Malaika wa BWANA akamtokea,katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti;akatazama,na kumbe !kile kijiti kiliwaka moto,nacho kijiti hakikuteketea. Musa akasema, Nitageuka sasa,niyaone MAONO haya makubwa,na sababu kijiti hiki hakiteketei. " Kutoka 3:2-3

Musa alipata maono haya akiwa yupo macho. Kwa lugha nyingine Musa hakuwa amelala,Bali alikuwa U macho,ndiposa malaika wa BWANA akamtokea Musa katika mwali wa moto katikati ya kijiti kiwakacho pasipo kuteketea.

BWANA MUNGU alikuwa akimuandaa Musa kukaa katika mkao ambao NENO lake Mungu lipate nafasi ndani ya Musa.
Ndiposa,
Bwana akamfanyia Musa kama kituko vile cha kuwasha moto katika kijiti kisichoteketea. Kituko hiki kilimuandaa Musa kusikia sauti ya Bwana maana Musa alitekewa na mazingira,na BWANA akazungumza na Musa.

Mungu pia anaweza kuzungumza na wewe kwa njia hii ya maono kwa macho ya wazi wazi,akitumia kituko fulani ili aukamate moyo wako,na neno lake BWANA lipate nafasi ndani yako,kama vile alivyojifunua kwa Musa.

Hivyo ;
hiyo ni njia moja ya maono,ambapo mtu aliye rohoni akipata maono kwa njia ya macho ya wazi wazi.

02.MAONO KWA NJIA YA USINGIZI.

Hii ni njia ambayo mtu hupata maono akiwa amelala.
Njia hii ni njia ya pili ambayo maono hupitia kwa mlengwa akiwa amelala. Maono yanayopitia njia hii ya usingizi sio ndoto,Bali ni maono.Ipo tofauti kati ya MAONO na NDOTO,lakini hapa nazungumzia MAONO na wala sio ndoto.

Tunasoma;
" Kwa hiyo Eli akamwambia Samweli,Enenda,kalale;itakuwa,akikuita,utasema,Nena,BWANA;kwa kuwa mtumishi wako anasikia.Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.BWANA akaja,akasimama,akaita vile vile kama kwanza,Samweli ! Samweli ! Ndipo Samweli akasema,Nena BWANA,kwa kuwa mtumishi wako anasikia." 1 Samweli 3:9-10

Haleluya...

Biblia inasema BWANA alimuita Samweli mara tatu,na kila Samweli alipoitwa,alimkimbilia kuhani wake Eli akidhani ya kuwa Eli amemwita,kumbe alikuwa akiitwa na BWANA.

Eli naye hakutambua sauti ya BWANA kwa mara hizo zote tatu;BWANA alipomuita Samweli,kwa sababu siku zile NENO LA BWANA lilikuwa adimu na wala hapakuwa na mafunuo dhahili ( 1 Samweli 3:1).Hivyo hata kuhani Eli hakuwa na mafunuo dhahili ndio maana hakuweza kuitambua sauti ya BWANA kwa urahisi.

Haleluya...

BWANA alimuhitaji Samweli aende kulala ndipo BWANA ajifunue kwake,kama tulivyosoma hapo juu,Samweli anaambiwa aende kulala tena ili BWANA apate nafasi ya kujifunua kwake.

BWANA hakujifunua kwa Samweli katika ndoto,Bali BWANA alijifunua katika MAONO.
Samweli hakuwa akiota ndoto,Bali alienda kulala ndipo BWANA akajifunua;maana tunasoma;

"...Basi Samweli akaenda AKALALA mahali pake.BWANA akaja,AKASIMAMA,akaita..." (1 Samweli 3:9-10)

Tunaposoma ;
"..BWANA akaja, akasimama..."
maana yake BWANA alijifunua katika maono. Lakini alijifunua pale Samweli alipokuwa amelala.

Swali moja ambalo waweza kujiuliza kama vile mimi nilivyojiuliza,ni kwamba;
*Je kwa nini BWANA hakujifunua kwa Samweli pale alipomuita Samweli kwa mara ya kwanza?

Au,
* Kwa nini BWANA alimuhitaji Samweli amjibu kwamba " Nena, BWANA ;kwa kuwa mtumishi wako anasikia"ndipo BWANA aanze kujifunua na kuanza kunena na Samweli,na asinene naye tu hivyo hivyo?

Umeelewa hapo?

Haleluya...

Ok,
Ndiposa nikapata JIBU,kwamba;
BWANA alihitaji Samweli afungue moyo wake ili neno lake BWANA likapate nafasi,maana kuanzia hapo Biblia inasema ;
"Samweli hakuliacha neno BWANA lipotee/lianguke chini" ( 1 Samweli 3:19)

Siku ya leo,BWANA huzungumza nasi kwa maono pia,lakini BWANA anatuhitaji tufungue mioyo yetu kwanza na kuwa tayari kusema " Nena nasi,kwa kuwa sisi watumishi wako tunakusikia"
Tukifaulu kuifungua mioyo yetu,neno la BWANA litapata nafasi ndani yetu.

Alikadhalika kupitia njia hii ya maono kwa njia ya usingizi,Tunamuona Yohana (Yohana mtume wa Yesu) alipokuwa katika kisiwa cha Patmo siku ya Bwana. Biblia inatuambia;

" Nalikuwa katika Roho,siku ya Bwana ; nikasikia sauti kuu nyuma yangu,kama sauti ya baragumu," Ufunuo 1:10

Biblia inaposema "....Nalikuwa katika Roho..." ina maana kuwa Yohana hakuwa na ufahamu wa kawaida,yaani akili za Yohana zilikuwa hazina matunda,Bali roho yake ndio ilikuwa hai,halisi,roho yake ilikuwa " active''/roho yake Yohana ilikuwa ikizungumza na BWANA.

Sikia;
Mtu akiwa Rohoni,akili hufa.
Na ndio maana njia hii ya MAONO hujulikana kuwa ni maono kwa njia ya usingizi,maana katika usingizi ni nusu ya kufa,lakini roho huwa halisi,sababu roho hailali,kinacholala ni akili tu.

Haleluya...

Tazama hapa;
"Nami nilipomwona,nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa..." Ufunuo 1:17

Maono haya aliyoyaona Yohana yalikuwa makubwa sana. Yohana alikuwa kama mtu aliyekufa,kwa sababu alikuwa kama amelala,Akili zake hazikuwa na kazi tena,Bali roho yake ilikuwa hai.

*Kumbuka nazungumzia MAONO yaonekanayo kwa njia isiyo ya macho ya wazi wazi./Njia ya usingizi.

Haleluya...

Yohana hakuwa anaota,Bali alikuwa akipata MAONO kwa njia ya roho yake,maana pale tusomapo kwamba Yohana alikuwa kama mtu mfu,maana yake akili,utashi,fahamu zake hazikuwa hai Bali roho tu ndio ilipata nafasi ya kuona...

ITAENDELEA...

*Usikose kabisa fundisho lijalo mahali hapa.

*Kwa huduma ya maombi na maombezi,piga;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Comments