MAUAJI KANISANI MOMBASA KENYA WAKATI WA IBADA LEO

Watu wawili mwanaume na mwanamke wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa baada ya watu wasiofahamika wakiwa na bunduki walifyatua risasi ndani ya kanisa la Joy Jesus maeneo ya Likoni karibu na mji wa bandari ya Mombasa nchini kenya wakati wa ibada jumapili ya leo.

Kwa mujibu wa afisa polisi wa mji wa Likoni Robert Mureithi amesema mtu huyo akiwa na bunduki alifyatua risasi ovyo kanisani humo kisha kukimbia, ambapo majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu ingawa haijaelezwa wamejeruhiwa kiasi gani. Mpaka sasa haijajulikana waliyehusika na tukio hilo ingawa kutokana na mashambulio ya mfululizo, kuna uwezekano wa kundi la Alshabaab kuhusika na shambulio hilo.

Ingawa pia katika mji wa Mombasa kumekuwa na tabia ya waumini wa dini ya kiislamu wenye imani kali kutotaka wakristo wawepo katika mji huo ikiwa pamoja na mji wa Mombasa kujiondoa kwenye jamhuri ya Kenya.Kwa mujibu wa kamanda Mureithi amesema mpaka sasa usalama umeimarishwa katika eneo hilo na jeshi hilo limeanza uchunguzi kubaini waliohusika na shambulio hilo.

Ni hivi majuzi polisi mjini Mombasa waliwakamata watu wawili wakiwa ndani ya gari na mabomu waliyoyatengeneza ndani ya gari hilo ikielezwa kwamba mabomu hayo yalikuwa na uwezo wa kuharibu majengo makubwa. Tayari tahadhari imetolewa nchini humo kuhusiana na matukio hayo ambayo yanaweza kusababisha maafa makubwa nchini humo, hivyo watu wametakiwa kuwa waangalifu.

SAMAHANI PICHA ZIFUATAZO NI MBAYA

Damu zikiwa zimetapakaa kanisani.
Mmoja wa majeruhi akipata matibabu hospitalini © standarddigital news Chanzo:Gospel kitaa   

Comments