MOYO WA MWANADAMU HAUNA TOFAUTI NA KIINI CHA YAI

''Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima -Mithali 4:23''. 

Ukilitazama yai lina vitu vitatu Gamba, nyama na kiini, Kwa hivyo Gamba na nyama hukificha kiini ambacho ndicho chenye thamani, kadhalika katika mwili wa mwanadamu, kuna ngozi nyama, ndipo unaupata 'MOYO', japo sijagusia habari ya mifupa, bali nimechukua vitu ambavyo vinaendana na Yai, kwa hivyo mwanadamu anapo hitaji KULA YAI HUTAZAMIA KIINI, 

Na  Abel Suleiman Shiriwa
maana hata kifaranga hakipatikani pasipo kiini, hata unapokuwa na kwasha kooo, au sauti yako si nzuri katika uimbaji, ina kwaruza basi unashauriwa kula yai, lakini unachokimeza ni kiini na si gamba wala nyama ya yai, 

Nyoka na wadudu wengine ambao hula mayai, wao nao hutafuta kiini kisha kulitema gamba kwa kuwa halina thamani kwao.

Kadhalika hata wewe mwanadamu, moyo wako ndiyo kiiini ambacho kinatafutwa kiweze kuliwa, yakupasa sana kuulinda moyo wako, 

kwa kuwa mwili wako hauna thamani kama moyo, hata kama wewe ni mzuri kiasi gani, lakini kama moyo wako si mzuri basi thamni yako haipo tena, 

LINDA SANA MOYO wako wadudu wasije kuutafuna, Wachawi, mahasidi, Wasengenyaji,wauaji, wazinzi, nk. wote hao wanautafuta moyo wako.

 hivyo usije kuwapa nafasi ya kuula moyo wako, bali Moyo wako mkabidhi Mungu pekeee. 

  ''Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;-Mithali 3:5''

waache wauchezee mwili yaani ngozi na nyama, lakini wasithubutu kuuchezea moyo wako, maana ndicho kiini cha Thamani.

MUNGU akubariki sana.

Comments