Mungu wetu
 ni Mungu wa kuinuliwa na kusifiwa na kila mtu. Mungu wetu amekuwa 
akifanya matendo makuu pkwa kupitia huduma ya RGC Miracle Center chini 
ya Mtume Peter Nyaga. Tumeona watu wengi wakiokolewa katika mikutano 
mbalimbali inayofanywa na mtumishi wake na mtiwa mafuta Mtume Peter 
Nyaga. Mungu amekuwa akisikia maombi ya mtumisjhi wake na kuwaponywa 
wagonjwa na wenye shida mbalimbali, mapepo yamekuwa yakiwatoka walio 
wengi na kuwaacha wakiwa huru. Mungu ameleta kicheko na furaha katika 
familia nyingi kwa kupitia mtumishi wake Mtume Peter Nyaga. Kazi ya 
Mungu inaonekana machoni mwa walio wengi kwa njia ya ishara na miujiza.

Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe
Kanisa
 la RGC Tabata Chang'ombe limekuwa bega kwa bega na waimbaji wa nyimbo 
za Injili Tanzania kwa kazi ya Bwana. Waimbaji hawa wanatoka katika 
makanisa mbalimbali lakini wameamua kuungana na Mtume Peter Nyaga 
kufanya kazi ya Bwana. Hakika huduma yao ya uimbaji imefanyika baraka 
katika mikutano na semina zinazofanywa na kanisa hili. Mungu azidi 
kuwalinda waimbaji hawa na kuwapa nyimbo zingine nyingi zenye kugusa 
nafsi za watu na kuwaokoa.
Tuone baadhi ya waimbaji hawa wakifanya kazi katika moja ya mkutano uliofanywa na kanisa la RGC Tabata Chang'ombe

Kulia ni Neema Gasper

Christina Matai akimtumikia Mungu siku hiyo

Christina Matai


 Tumaini Njole

  Tumaini Njole

Kenyatta

chanzo: Neema Gasper blog

Comments