![]() |
Mtume. Peter Rashid Abubakar |
Mtume Peter Rashid Abubakar ambaye ndiye
mwanzilishi wa huduma ya Glory to God Miracle Center(House of Prayer For
All Nations) Tanzania jijini Dar es Salaam amelionya kanisa akiliambia umetokea ujinga wa
kutumiana masage zikisema meseji hii tumia watu 12 au 20 imetoka kwa
Tb. Joshua!!!???
Alihoji Tb. Joshua yeye ni nani!!? Mbona ni mtumishi
wa MUNGU kama mimi tu!
Akiongea huku akinukuliwa na Maisha ya ushindi blog alisema
watu wengi kanisani hapa kwangu
wanafunguliwa wasio na watoto; Kazi; etc wanapata kwa jina la YESU.
Alisema nimeombea wangapi waliokwenda kwake Tb. Joshua ambao
hawakuponywa au kufunguliwa na niliwaombea na YESU KRISTO akawaponya.
Aliuliza je YESU wa Tb. Joshua na mimi ni tofauti? YESU KRISTO mwenyewe kwa kauli
yake anasema YEYE HABADILIKI. YEYENI JANA NA LEO NA HATA MILELE.
Alisema huo ni
USHAMBA WA KIROHO AU NI UKIRO WA KIROHO(UKIRO=U-Ukosefu wa K-Kinga wa R-
Roho) ni sawa na UKIMWI= Ukosefu wa kinga za mwilini).
Alisema Yeremia
17:5-6. Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na kumfanya kinga
moyoni mwake.
Kwa imani yenu hiyo alisema Mbona wenye karama ya uponyaji
na matendo ya miujiza mbona nipo mimi hapa? Na wengine wengi tu Dar es
salaam au Tanzania.
Hizo pesa nyingi za nauli mnazopoteza kwenda Nigeria na
kurudi huko si mniletee mimi nizijengee kanisa? Au pelekeeni wazazi wenu
wanaokufa na njaa zikawasaidie?
Wengine hata uwanja wa kujenga hamna?
Alimalizia kwa kusema POLENI WATANZANIA WENYE IMANI HIYO KATIKA JINA LA
YESUUU!!!
KAMA NI TB. JOSHUA NIPO HAPA MBEZI MWISHO JIJINI DAR ES SALAAM
NAULI MIA TANO KWENDA NA KURUDI ELFUUU. EMEEEEEEEE!!! Kanisa lote
liliitikia Emeeeeeeee!
![]() |
Comments