NILICHOKIONA KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI

Haleluya...
Hivi karibuni nilitembelea hospitali ya taifa,Muhimbili.Nikaamua na kucheki afya yangu,nikafanyiwa na baadhi ya vipimo vya damu,ikawa ni sawa kabisa,yaani ni Haleluya tu.
Nilipokuwa hospitalini,nikagundua kwamba wagonjwa wengi si wagonjwa Bali ni nguvu za mapepo tu hata wakawa wagonjwa.
Yaani wengi husumbuliwa na nguvu za giza zinazowafanya wajione kwamba ni wagonjwa,na pia waonekane wagonjwa.
Kumbe!
Sasa hali ikiwa ndio hiyo,basi ipo kazi ya kufanya kuwakomboa hawa ndugu.Maana wengine walikuwa hawaitajiki operation yoyote ya daktari,wala kupewa madawa yoyote yale,
Ile isipokuwa ni kuombewa tu na kisha watoke wakiwa wamepona kwa uweza wa jina la Yesu Kristo.
Mimi nafikiri sisi watumishi tusibakie madhabahuni tu,SASA TUTOKE NA KWENDA MAHOSPITALINI watu wakampokee Yesu huko huko hospitalini.
Zipo roho za watu zinateseka wakati sisi tupo,HII HAIWEZEKANI!
Muhimbili hali inatisha ndugu zangu. Si wakina mama wala akina baba wala watoto,wote wamelundikana Muhimbili wakihitaji msaada wa kupona magojwa,ILA DAWA NI JINA LA YESU TU.
Kuna kipindi nilimuambia daktari kwamba najisikia vibaya,naye akaniambia inabidi nichukue vipimo ili kupitia vipimo hivyo wagundue tatizo ,ndipo wanipe dawa.
Sasa hii ni tofauti na Yesu wetu,ambaye Yeye haitaji kuchukua vipimo vyako ndipo akupe dawa,Bali kwa UWEZA WAKE MKUU,NI UPONYAJI SAA ILE ILE.
Ipo kazi ya kufanya watumishi wa Mungu TWENDENI MAHOSPITALINI TUKALITANGAZE JINA LA BWANA YESU,MUNGU AISHIE,MUNGU ALIYE HAI.
UBARIKIWE.
                        By Mtumishi Gasper Madumla

 mtumishi Gasper Madumla

Comments