![]() |
Mtumishi wa Mungu Alex Emmanuel Bubelwa |
Mwaka 1992, nikiwa darasa la pili
nilianza kuugua ugonjwa wa kifafa. Nilikuwa nikianguka mara kwa mara,
kichwa kilikuwa kinaniuma kwa namna ya kutisha, siku zote nilikuwa na
kizunguzungu. Shuleni hata nilipofanya kosa nilikuwa sichapwi, walimu
walijiadhali nisianguke mikononi mwao!
Wazazi walinipeleka hospitali lakini nafuu ilikuwa inapatikana kwa kipindi kifupi kisha hali inarudia vile vile!
Baadae nilipelekwa kwa mpiga ramli (mganga). Mganga alituambia kuwa nililogwa na Shangazi, kisha akanipa hirizi na madawa.
Huyo mganga alinitibia kwa miaka 3, kisha akafa kabla sijapata nafuu!
Nilipelekwa kwa mwingine, nikatibiwa
mwaka mzima bila mafanikio, tulilazimika kutafuta mwingine kwa sababu
aliwafilisi wazazi wangu, gharama zake zilikuwa kubwa.
Nilipelekwa kwa mwingine, alinitibia tangu 1997 -1999. Nilipigwa chale zisizo na idadi, sikupata nafuu!
Mwanzoni mwa mwaka 2000 Mjomba alinileta Dar, nilikutana na Watumishi wa Mungu nikamwamini YESU.
Yale yaliyoshindikana kwa miaka minane kwa wachawi, YESU ALITUMIA DAKIKA MOJA KUNIWEKA HURU KABISA!
NILISHASEMA NA NITASEMA TENA: KATIKA MAISHA YANGU YALIYOBAKI HAPA DUNIANI, HAITATOKEA NIKAMUACHA YESU!
Neno la Mungu linasema 'Injili;
kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye'. Na
Mungu hana ubaguzi. Mtu akiamini Mungu anamuokoa. Hata leo yuko tayari
kukuokoa na kukuponya nawe msomaji. Kama unahaja yoyote ukiamini Yesu
atatenda.
Ubarikiwe.
Comments