Obama akutana na Papa Francis


 Papa Francis akutana na Obama
Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.
Rais Barrack Obama wa Marekani amekutana na na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, katika makao yake makuu huko Vatican. Obama ameambatana na waziri wake wa maswala ya kigeni John Kerry.

Hii ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.

Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.

Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
 
 Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili Vatican

Papa Francis amekuwa mstari wa mbele akipigania kubadili sera na mtazamo wa Kanisa na viongozi duniani kuhusiana na mikakati ya kupunguza tofauti kubwa baina ya maskini na matajiri duniani .
Aidha viongozi hao wawili wanatazamiwa kujadili hali ilivyo Nchini Ukraine, na swala la upatikanaji wa amani mashariki ya kati.
  Rais wa Marekani, Barack Obamaakisalimiana na mmoja wa padri Georg Ganswein alipowasili Vatican
Mwafaka baina ya mitazamo tata ya wawili hao kuhusiana na maswala ya uavyaji mimba, matumizi ya dawa za kupanga uzazi na ndoa ya jinsia moja pia inatarajiwa kuwa kati ya mada itakayojadiliwa .

Baada ya kukutana na papa rais Obama ameratibiwa kukutana na rais wa Italia Giorgio Napolitano mbali na waziri wake mkuu Matteo Renzi.

Obama amezuru Roma baada ya siku tatu ya mazungumzo na viongozi wa Uholanzi na Umoja wa ulaya huko Brussels ambapo mada kuu ilikuwa ni taharuki inayokumba eneo zima la Crimea na Ukraine

baada ya Urusi kutuma vikosi vya jeshi lake katika jimbo hilo .
Obama tayari ameanza kuandaa mikakati na vikwazo zaidi dhidi ya Urusi kwa kuingia Ukraine.

Obama ameambatana na waziri wake wa maswala ya kigeni John kerry.

Comments