RAIS WA KOREA KASKAZINI AAGIZA WAKRISTO 33 KUNYONGWA

Rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini.©Manlycurls
Wakristo duniani wametakiwa kuomba kwa ajili ya mabadiliko ya ki Mungu katika taifa la Korea Kaskazini ambako Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un ameagiza kunyongwa kwa wakristo wapatao 33 wa nchini humo ambao wanadaiwa kupokea msaada wa kuendesha makanisa ya siri kutoka kwa mmisionary wa Korea ya Kusini Kim Jong Wook.

Kwa mujibu wa Rais wa shirika la Open Door la nchini Marekani bwana David Curry katika ujumbe wake jumatatu hii amesema Korea kaskazini ni nchi inayoshika namba moja katika orodha iliyotolewa na shirika hilo kwa nchi ambazo wakristo wanaishi katika hatari kubwa duniani ikiwa katika nafasi hiyo kwa miaka 12 mpaka sasa. Amesema kwasababu nzuri kabisa unapoona manyanyaso yanazidi katika taifa ndipo moyo wa kumuhubiri na kumtangaza Kristo unapoongezeka hivyo kuwataka wakristo kuungana naye kuliombea taifa hilo.

Wiki iliyopita moja ya gazeti la Korea kusini limeripoti kwamba Rais Kim Jong Un ametoa maagizo ya kunyongwa kwa wakristo hao 33 baada ya kugundulika kupokea msaada huo ambao ni wakujenga makanisa 500 ya siri kitu ambacho ni kinyume cha sheria nchini humo kwa kujiunga katika vitendo vya kidini adhabu yake ikiwa ni vifungo ama kunyongwa hadharani katika taifa hilo la Korea ya kaskazini.
Rais Kim akiwa na marehemu mjomba wake Jang aliyenyongwa mwaka jana.©kyodo News
Shirika la Open Doors limewaomba wakristo kuomba rehema kwa watu wote ambao wamehukumiwa kifo huko Korea ya kaskazini, pamoja na wamisionari wengine ambao wameshikiliwa nchini humo kutokana na imani yao, ikiwa pamoja kuliombea taifa zima la Korea kaskazini na Rais wao kwamba Mungu awape mioyo myepesi na kumrudia yeye.

Mwaka jana Rais huyo aliyerithi nafasi kutoka kwa marehemu baba yake aliagiza kunyongwa kwa mjomba wake Jang Song -Thaek ambaye alikuwa mtu muhimu sana kwa taifa hilo kutokana na historia yake katika utawala na mambo ya siasa kwakosa la kudaiwa kutumia vibaya madaraka yake.
Marehemu Jang mjomba wa Rais Kim akiwa chini ya ulinzi mara baada ya kukamatwa. ©AFP/Getty Images
Chanzo CP

Comments