SHIKA MAAGIZO YA BWANA NA MVUA ZA MIUJIZA ZINYESHE KWAKO KWA WAKATI WAKE,

Na Mwinjilisti John Chinyuli
Baraka zipi unazisubiri kwenye maisha yako,
baraka zipi zimekawia kwenye maisha yako,
niyapi ambayo unataka Mungu akufanyie kwenye maisha yako,
je ni kwenye magojwa au kazi au masomo au ndoa au biashara ni eneo lipi kwenye maisha yako unataka Mungu ashushe baraka zake ,alete mvua za miujiza zishuke kwenye maisha yako,majibu ya shida zako maandiko yanasema ...."kama mkienenda katika amri zangu na kushika maagizo yagu,na kuyafanya ndipo nitazinyesha mvua zenu kwa nyakati zake....Mambo ya walawi 26:3-4"  

amina ,mpendwa hebu ujumbe huu ulete majibu ya shida zetu pale ambapo tumekwama tena kwa wakati wake,amua leo tena fanya maamuzi binafsi ya kushika MAAGIZO ya Bwana na tena si tu kuyashika na kuyafanyia kazi kuishi maisha ya kumpendeza Mungu,amua kuacha dhambi naye Mungu atakuwa rafiki yako na kukupigania kwenye kila hali nataka nikwambie majibu yashida zako yapo kwa Yesu tu,ng'ang'ana kwa Mungu,mwisho wa shida zako ni sasa,chochote kinachokusumbua ktk jina la Yesu amua kuacha mabaya na kumuomba Mungu naye anasema atazinyesha mvua kwa maana ya baraka au miujiza ua majibu ya shida zako kwa wakati wake,nataka nikwambie unajichelewesha mwenyewe kama unaendelea kutenda mabaya na huku unataka Mungu akupiganie kwenye maisha yako,kuwa mjanja tambua fulsa zipo kwa Mungu kama tu utaamua kuacha mabaya tena biblia inasema.....baraka humkalia mwenye haki kichwani..mithali 10:6,

kazi kwako fanya maamuzi acha kuteseka mtanzaniaa.amina amina jumapili njema ......aliye na akili moyoni mwake atapokea agizo mitahali 10:8..

pokea agizo lakuacha mabaya na mvua za baraka zinyeshe kwako kwa wakati ..

KILA ALIDHARAULIE NENO HUJILETEA UHARIBIFU..MITHALI 13:13,...NI HERI TUAMBIANE UKWELI HATA KAMA VIPI...MAANA NDIO SULUHISHO LETU..SIFA NA HESHIMA KWA BWANA PEKE YAKE

MUNGU akubariki sana ,

 By Mwinjilisti John Chinyuli 
 0767 592989/0712 592989

                                      ***sharing is care***

Comments