Mchungaji ADRIANO MAKAZI, Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe akianza kufundisha Neno la BWANA |
Utangulizi: Leo tutawafuatilia adui zetu mahali popote walipo na
tutarudisha nyara walizochukua kutoka kwetu kwa jina la YESU, tunaamua
kuwafuata kupigana nao na kurudisha kila walichokichukua kwetu kwa jina la YESU
Isaya 42:22 “Lakini watu hawa ni watu
walioibiwa, wamekuwa mawindo wala hapana okoaye, wamekuwa mawindo wala hapana
asemaye rudisha”
Isaya
alikuwa anaona maono ya Bwana na katika maono aliona kuna watu walioibiwa na
kutekwa na katika majira hayo wachawi walikuwa wanaweza kufanya lolote na
hakuna aliyewakataza, nyakati zile watu walikuwa hawana jinsi maana hakuna
aliyesema RUDISHA.
Biblia inasema
watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa,
maana yake kuna watu walioibiwa nyota zao , akilia zao , ndugu zao ,
mali zao na nyuso zao, watu wengine
wameibiwa vichwa. Kuna mtu anaweza kutekwa kama anafanya biashara akili na
nyota yake ikaanza kutumiwa na mtu mwingine na yeye hawezi kufanya jambo lolote
kwa uwezo wake binafsi, unashangaa mtu anafanyiwa mambo ya ajabu lakini anakua
hana uwezo hata wa kuhoji kwasababu nyota yake imeibiwa. .Leo tunawafuata adui zetu maana tunaye
kiongozi YESU KRISTO na nguvu tunazo na hakuna anayeweza kutuzuia tukiwa na
kamanada Yesu . Kwa nyakati hizi
tunazoziendea lazima wachawi waaibishe na hawatakuwa na la kusema kwa jina la
Yesu kwa maana tunawafuata kwa uwezo wa jina la Yesu.
Leo tunafanya
maandamano ya rohoni na kuwafuatilia maana sisi ni majeshi ya Bwana na tunajua
kila mahali na kila kitu, kwa kuwa shetani hana kitu kwa maana alipoasi
mbinguni alinyang’anywa vyote hivyo naye anachofanya ni kuiba vya wengine ili avitumie
, lakini leo tunamfuata na kumnyang’anya vyote , katika jina la YESU.
Neno rudisha ni
silaha hatari linapotamkwa lazima kuzimu
nzima itaharuki na kuwaka moto, kwa hiyo tunapowaendea lazima tuwanyang’anye
vyote. Shetani anawateka na kuwaweka watu gerezni na ndo maana mtu anapokuwa
ibadani anaanza kusinzia kumbe shetani katangaza kuwa wafungwa wake wote lazima
walale. Unapokuwa gereza la rohoni unakua unapanga mipango yako lakini haiwezi
kutekelezeka kwa sababu uko gerezani unapopanga nifunge na kuomba inashindikana
kwa maana tangazo linatoka kuzimu wafungwa wangu wawe na hamu sana ya chakula.
Kwa hiyo huwezi kutoka gerezani mpaka atokee wa kusema rudisha. Na mchana wa
leo utaona tunaposema njoo magereza ya kuzimu yanapsasuka na kuvunjika vipande
vipande na watu wa Mungu wanaachiliwa.
Wanajua kuna
milango mingine inayofunguka kumbe ni mitego ya shetani anakutega ukiingia
anafunga. Kwa hiyo kuna uwezekano kabisa mtu kuwa gerezani ndiyo maana unaweza
akapanga kuomba lakini ukashindwa kumbe mkuu wa gereza(shetani) ametangaza
wafungwa wote walale. Mahali kama hapo unatakiwa kutumia neon njoo na sio toka.
Unapoita njoo inakuwa hatari kwa shetani kwa maana anajua mwenyewe amekuja
lakini neno toka halimsumbui kwa maana
hawezi kuuacha mwili peke yake yeye ndo ameumiliki, kwahiyo neno njoo
linasababisha yule mfungwa aliyefungwa kwenye gereza la kishateni kuchomoka na
kuwa huru kabisa.
IBRAHIMU
ALIRUDISHA BAADA YA KUFUATA
Mwanzo 14:8-16 Utaona wafalme wa Sodoma
na Gomora walitegewa mashimo na kunaswa
kwa maana hawakujua mbinu za adui zao kuwaita mahali pale, ndo maana kuna watu
wameanza vizuri kumtumikia Mungu na baadae wakanaswa kwenye mashimo ya uharibifu na sasa
ni watumishi wa joka(shetani) na wanaona aibu kusema lazima watu walio nje wanajua
yeye ni mtumishi wa Mungu lakini wameshamuacha Mungu siku nyingi. Heri wewe uliyeamua kukimbilia ufufuo na
uzima kwa maana utapewa maarifa ambayo
ni Roho Mtakatifu na utawafuata ndugu
zako na vyote vilivyoibiwa kwa Jina la
Yesu.
MGANGA WA
KIENYEJI ALIPOFUATWA NA KUHAMISHWA NA MAJESHI YA BWANA
Wakati
tulipokuwa Ubungo mwaka 2004 kuna mganga
mmoja wa kienyeji anaitwa Lamba lamba hapo jirani sasa siku moja
tukaamua kwenda kumuhamisha
mahali pale na tulikwenda kama wateja wake.Tulipofika tukamwambia sisi
watatu
tunakaa pomoja ila tumepotelewa na hela na kila mtu anakataa sasa
tunaomba utuambie nani amechukua akasema sawa, akaanza kupiga manyanga
yake na
baada ya muda akasema tokeni kwangu kwa maana mmekuja kwa shari na
akasema kama
mkiamka asubuhi hai siyo mimi sio mganga lazima mtakufa , na sisi
tukamwambia
kama ni watumishi wa Mungu ikifika kesho bado uko mahali hapa unakufa.
Kesho
yake asubuhi na mapema akaamka na kufungasha kila kilicho chake
akaondoka. kuna
watu wanaoharibu kazi za watu , hii inatufundisha wakati mwingine lazima
tuwafuate sio kuomba pakee.
Usidhani
Tanzania tulipata Uhuru bila kupigana vita siyo,kwa kuwa baba wa Taifa alikuwa
mtu wa rohoni upande wa giza kwa hiyo kuna vitu alivyofanya rohoni na kuwaondoa
wakoloni ndiyo maana vitu vile alivyofanya vinatupeleka pabaya utaona tuna
rasilimali nyingi lakini hatuwezi kuzitumia wenyewe na tunabaki masikini na
omba omba kwa mataifa mengine kwasababu ya msingi wa giza uliowekwa na
waanzilishi wa taifa.
SHETANI
ALIONDOKA MBINGUNI BAADA YA VITA KUPIGANWA
Ufunuo 12:7-16 , Vita ilipiganwa
mbinguni na Lusifa(Shetani) akatupwa chini. Hii inatufundisha kwamba hakuna
kumiliki bila kupigana, huwezi kuolewa bila kupigana, huwezi kujenga bila
kupigana, huwezi kusoma bila kupigana, huwezi kupata hehima bila kupigana, leo
katika ulimwengu wa roho unadharauliwa kwa sababu unapigwa, hata Rebeca alikuwa
na mapacha tumboni walioanza kupigana tumboni wakishindana nani amtumikie
mwingine. Hata wewe lazima upigane ndo maana wenzako wanaenda kwa waganga wa
kienyeji wanapigana na kupata vyeo ndio maana wanapopita barabarani wanapigiwa
ving’ora kwa maana wamepigana na kushinda rohoni.
Katika mapigano
kuna kujeruhiwa au kufa lakini sisi
katika mapigano haya hatuwezi kufa kwa maana YESU alishakufa kwa ajili yetu ila
adui zetu lazima wafe.
Maombi
ya kuwafuata adui na kurudisha ulichoibiwa
Kwa
mamlaka ya jina la Yesu ninawafuata adui zangu wote walioiba nyota yangu, fedha
zangu, ustawi wangu, heshima yangu, kibali change na vyote nilivyoibiwa kwa
jina la Yesu. Ninawateketeza adui wote wa rohoni, adui majini, majoka, mizimu
na wengine wote ninawateketeza kwa jina la Yesu na ninaangamiza uweza wenu
wote.
Ninaamuru
kila ambacho mmeniibia anza kurudisha kwa jina la Yesu, ninaamuru vyote
vilivyoibiwa njooo kwa jina la Yesu( anza kuita vitu vyote ambavyo unahisi
shetani ameviiba katika maisha yako kwa jina la Yesu)![]() |
Ufufuo na Uzima,Tanganyika parkers Kawe |
Comments