BWANA YESU
asifiwe.
Karibu tena
tujifunze jambo muhimu kuliko yote wanalotegemea wanadamu wote yaani TAJI YA
UZIMA, ambapo taji hiyo wanaipata walioshinda ya dunia na kuingia UZIMA WA
MILELE kupitia YESU KRISTO.
1 Korintho
9:25-Na kila ashindanaye
katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji
iharibikayo; bali sisi tupokee TAJI ISIYOHARIBIKA
-Heri mtu
yule astahimiliye majaribu majaribu ya dunia maana akishinda atapokea TAJI YA
UZIMA.
Yohana 3:16
inatuonyesha mwanzo wa taji ya uzima ambapo MUNGU anamtoa BWANA YESU kwa ajili ya
kila mwanadamu ambaye atapenda kuwa UZIMANI.( Kwa maana jinsi hii MUNGU aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa
milele.)
-Uzima ni
kitu cha kwanza.
-Kila mtu
anahitaji uzima.
-Wanadamu
wote walikuwa wamepungukiwa na utukufu wa MUNGU, lakini kwa mmoja tu(YESU
KRISTO) tunapata uzima wa milele.
Yakobo 1:12.
-Heri mtu astahimiliye
majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea TAJI YA UZIMA, BWANA
aliyowaahidia wampendao.
Tunatakiwa tupate
uzima wa milele, ila majaribu yapo lakini atakayestahimili mpaka mwisho wa
maisha yake ataipata taji ya UZIMA WA MILELE.
-Duniani ni
njia ya tu ya kwenda katika makazi ya milele.
Makazi ya
milele yapo ya aina mbili.
1. Makazi
ya uzima wa milele.
2.
Makazi
ya mateso milele.
Najua kila
mtu anahitaji UZIMA WA MILELE. Na uzima wa milele unapatikana katika KRISTO
YESU pekee(Yohana 14:6, NA PIA Matendo
4:12- inayosema ‘’Wala
hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini
ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.’’).
Uzima wa
milele ni muhimu sana, na ni hakika kila mtu anamhitaji BWANA YESU ili apone
kutoka kwenye mikono ya shetani.
Asante sana
BWANA YESU kwa uzima wa milele.
Ufunuo 2:10.-
Usiogope mambo yatakayokupata; tazama, huyo Ibilisi atawatupa baadhi yenu
gerezani ili mjaribiwe, nanyi mtakuwa na dhiki siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa,
nami nitakupa TAJI YA UZIMA.
-Wengi sana
wanaompenda MUNGU, hupenda baraka zake tu, lakini wakipata majaribu kidogo
hugeuka na kuonyesha kabisa kwamba hawampendi MUNGU.
-Tunaweza
kuwa na furaha wakati wa dhiki, kama tu ROHO MTAKATIFU yuko ndani yetu.
-Taji ya
uzima tunaipata katika KRISTO tu.
BWANA YESU
anasema katika Ufunuo 22:12-13’’Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu
kama kazi yake ilivyo.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.
TUMPELELEZE
NANI HABARI ZA MBINGUNI?
Tumpeleleze
nani habari za mbinguni?
Tumpeleleze
nani habari za uzima?
Tumpeleleze
nani habari za uponyaji?
Tumpeleleze
nani habari za mafanikio?
Tumpeleleze
nani mambo ya mbinguni?
YESU NDIYE
WA KUMPELELEZAAAAAAAAAAAAA.
YESU ndiye
wa kumpeleleza maana yeye anao UZIMA.
Songa mbele
na BWANA YESU ndugu.
Hakuna uzima
kwingine kokote ila kwa YESU KRISTO pekee.
Asante BWANA
YESU kwa uzima.
Asante YESU
unayeokoa.
Asante YESU
utupaye TAJI YA UZIMA.
Zaburi 16:11’’Utanijulisha njia ya uzima; Mbele
za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.’’
Kwa sasa naishia hapo,
MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea
BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu
kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana
makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani
aliko KRISTO BWANA.
mabula1986@gmail.com
Comments