TUMIA NENO LA MUNGU KUJIWEKA HURU MBALI NA KUTESWA NA NGUVU ZA GIZA.

Shalom ndugu.
karibu tujifunze.

Neno la MUNGU ni kweli inayodumu milele,
Neno linaumba.

Kwa neno la MUNGU tunakuwa huru mbali na nguvu za giza.
Ndugu zangu katika BWANA YESU kumbukeni kwamba shetani akitaka amtese mtu wa MUNGU huhakikisha mtu huyo hapati nafasi ya kumwomba MUNGU.

Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Waebrania 4:12.

Katika maombi ndipo neno la MUNGU ambalo li hai siku zote hutumika, na likitumika kuharibu mambo yote ya shetani.

Tumia neno la MUNGU katika maombi siku zote,

BWANA YESU kipindi akijaribiwa na shetani, alimshinda shetani kwa neno la MUNGU. BWANA alijibu hivi ''Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Mathayo 4:4''

Mpendwa omba maombi ya vita ukidai vyote ambavyo shetani aliviteka kipindi hujaijua siri hii.

Ahadi ya MUNGU kwako ni hii  ''Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni. Mathayo 16:19''
Mlazimishe aviachie na ataviachia.
BWANA ametupa mamlaka kuu sana. na kwa maombi ya vita mamlaka hiyo inatenda kazi. Biblia inasema hivi 
 ''Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.  Luka 10:19''

Silaha yako ya kumshinda shetani ni neno la MUNGU kupitia maombi. omba kwa mamlaka na shetani atakimbia, magonjwa yatakimbia, mikosi itakoma, balaa zitafutika na utakuwa mshindi siku zote .

Tunapigana vita katika ulimwengu wa roho  na kwa sababu MUNGU wetu ndio anamiliki kote huko sisi watoto wake siku zote tunashinda.''2 Wakorintho 10:4,5 (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika MUNGU hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO;'' 

Shetani huogopa sana neno la MUNGU, na kama utalitumia neno la MUNGU kwa ufasaha nakuhakikishia utakaa huru siku zote.

  ''Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.  Waefeso 6:10, 11

 Neno la MUNGU linatutaka 

1. Tuwe hodari katika BWANA.

2. Tuwe hadari katika kutumia nguvu za MUNGU.

3. Tuvae silaha zote za MUNGU ili tuweze kumshinda shetani.

4. Tuzipinge hila za shetani.

Ndugu zangu tuzingatie hayo hapo juu na tufanye maombi siku zote , maana sisi ni washindi na zaidi ya kushinda kwa YESU aliyetupenda.

Biblia inatuambia jambo muhimu na tena unatupa uhakika muhimu sana. inasema 
'' Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia. .1Yohana 4:4''

MUNGU akubariki sana.
  na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
                 MUNGU akubariki sana .
                  Ni mimi ndugu yako
                  Peter M Mabula
         Maisha ya Ushindi Ministry.
                   0714252292

Comments