UTHAMANI WA MAISHA YAKO UTAONEKANA PALE TU UTAKAPOACHA DHAMBI....!

    Na Mwinjilisti John Chinyuli
  • Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. - 1 Yohana 1:9
-----maisha ya dhambi ni zaidi ya ugonjwa wa akili---hata usipo soma...!inakuhusu--
  BWANA YESU akamwambia, ............. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.] - Yohana 8:11b

 SIKU HIZO ZINAKUJAGA UTAKAPOKUWAGA UNASEMA NINGE.... NINGE... NINGE..... BAHAT MBAYA zaidi MUDA HUWA HAURUDI NYUMA RAFIKI NAKUONA UNAFANYA MIZAHA NA MAISHA YAKO KAMA VILE UMEAJILIWA KAZ USIYOPEWA MSHARA NAONA UMEKAZANA KUYACHAKACHUA MAISHA YAKO HIVI HUOGOPI,

BWANA anasema kwamba kama ukiokoka na kutubu toba ya kwele yeye anasema.  ''Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. - Waebrania 8:12

Ndugu be serious acha ujinga ,shetanI hana huruma na mtu awaye yoyote kazi yake kutafuna tu atakaye tokeza mbele yake ambaye hajitambui,hayo maisha n ya kwako kwann wengine wakushikie maamuz ya maisha yako wanakuendesha tu,kazi yako kufuata mikumbo ya kishetan hata aibu huna,itakusaidia nn sasa,amua kuwa na misimamo ya haki,acha kutenda mabaya coz mwisho wa mabaya n aibu ,wajifanya msiri na michezo yako ya kichafu ya chini chin utakufa,acha dhambi mtanzania,nazungumza na wewe maamuzi yeyote ya kijinga unayoyafanya sasa utawajibika mwenyewe matunda yake yakianza kujitokeza,ok.

MUNGU akubariki na acha dhambi, tubu toba ya kweli na wasamehe wengine pia ambao walikukosea. Biblia inasema
'' Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu. - Mathayo 6:14,15.


  • Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. - Mambo ya Walawi 19:18 
 Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. - Zaburi 86:5 


Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu. - Mithali 3:3,4 

  • Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. - Luka 6:37

MUNGU akubariki kwa tafakari hii.
 By Mwinjilisti John Chinyuli

                    -----(Jesus Opeartion )----------

Comments