VIPENGELE 20 MUHIMU VYA MAOMBI NA MAJIBU YAKE.



BWANA YESU asifiwe.
karibu tuvipitie vipengele hivi 18 vya kuhusu maombi na majibu yake.
MUNGU akubariki.

1.  Maombi ni hali ya kuongea na MUNGU
Zaburi 4:3 "Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa BWANA atasikia nimwitapo." 
Ndugu mwite MUNGU leo kwa maombi ili upokee majibu yako.

2.  Maombi ni haki.
  Waebrania 4:16 "Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji." 
Ndugu uliyempokea BWANA YESU tambua kwamba maombi ni haki yako, yaani MUNGU atakusikia na kukujibu hata bila kupitia kuombewa na wengine.


3.  Twaweza kumkaribia MUNGU. 

Zaburi 65:2 "Wewe usikiaye kuomba, wote wenye mwili watakujia." 
Twende mbele za MUNGU kwa maombi .

4. Je MUNGU yuko tayari kusikia maombi yetu na kutujibu? 

Mathayo 7:11 "Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema je! si zaidi BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?". 
 MUNGU anajibu maombi, ni jukumu lako tu kuomba leo.


5.  Je kwa namna gani mahitaji yetu ya hutimizwa? 

Mathayo 7:7-8 "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona bisheni nanyi mtafunguliwa. Kwa maana kila aombaye hupokea naye atafutaye ataona, naye abishaye atafunguliwa." 

Hili ni neno la ufunuo, ni siri ya maombi na aina zake, ufunuo huu unasema hivi,
- kuna wakati wa kuomba yaani kumwomba MUNGU chochote.

-Kuna wakati wa kutafuta yaani kutumia mamlaka ya KRISTO iliyoko ndani yako kutafuta chochote katika ufalme wa MUNGU. mfano Tafuta nguvu za MUNGU kwa kufunga na utaziona zikitenda kazi katika huduma yako.

-Kuna wakati wa kubisha yaani kwa kutumia mamlaka ya KRISTO iliyoko ndani yako unagonga ndani ya mwili wa mgonjwa na ugonjwa unasikia na kukimbia, na mtu huyo anabaki huru, gonga kwa jambo lolote ambalo shetani amelishikilia katika maisha yako na umfukuze shetani ili ubaki huru.

Hizi ni siri kuu za maombi alizozisema BWANA YESU japokuwa kwa kanisa la leo wengi hukosea yaani hawahui ni wakati gani wa kuomba , kutafuta na kubisha. na wakati mwingine kwenye kuomba wengine wanabisha na kwenye kubisha wengine hapo ndipo wanatafuta.

Tutulie katika ROHO MTAKATIFU ili atusaidie kuomba inavyotakiwa.


6.  Jambo la muhimu kuomba ni hekima.

  Yakobo 1:5-8 "Lakini mtu kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU, awapeaye wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote, maana mwenye shaka nikama wimbi bahari lililochukuliwa na upepo na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani yakuwa atapokea kitu kwa BWANA. Mtu wania mbili husita-sita katika njia zake zote." 
Omba mpendwa.

7.  Kwa nijia gani MUNGU hatayasikia maombi yetu? 

 Zaburi 66:18-19 "Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, BWANA asingesikia. Hakika MUNGU amenisikia. Amesikiliza sauti ya maombi yangu." 
Ukiwaza maovu MUNGU hatakusikia maana dhambi ni chukizo mbele za MUNGU, jitakase kwanza ndipo upeleke mahitaji yako kwa MUNGU.


8.  Je MUNGU hukataa kusikiliza maombi? 

Mithali 28:9 "Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria hata sala yake ni chukizo." 
Kama hulitaki neno la MUNGU au sheria ya MUNGU hata maombi yako ni chukizo.
wengi hawapendi mambo ya MUNGU lakini wanataka MUNGU huyo huyo awajibu maombi yao, ni ngumu sana.
Wengi hawataki hata kusikia kanisa wala mikutano ya injili wala semina ya neno la MUNGU lakini wanataka MUNGU awajibu, ni ngumu sana.

9.  Tuombe kwa jina gani? 

Yohana 14:13-14 "Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu hilo nitalifanya ili BABA atukunzwe ndani ya mwana mkiomba neno lo lote kwa jina langu nitalifanya[Yesu]." 

Tuombe kwa jina la YESU KRISTO tu.
Hata kama utaomba maombi gani na kwa muda gani , lakini kama hujaomba katika jina la YESU KRISTO usahau kujibiwa .
MUNGU ameamuru tuombe katika jina la YESU KRISTO pekee. hakuna jingine.

10.  Usisahau kumshukuru MUNGU kwa kuyajibu maombi yako. 

 Wafilipi 4:6 "Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru hajazenu zijulikane na MUNGU." 
Kushukuru ni muhimu sana. usiache kushukuru baada ya kumaliza maombi yako maana hata hiyo nafasi ya kuomba ni MUNGU ndio amekupa. pia ukijibiwa ndio kabisa kushukuru kwako kuwe lazima. Shukuru kwa maombi na shukuru kwa sadaka pia yaani sadaka ya shukrani.

11. Tuombe mara ngapi kwa siku?

 Waefeso 6:18 "Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho mkikesha kwa jambo hili na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
Na tena 
1Wathesalonike 5:17 "Ombeni bila kukoma." 
Maombi hayana kipimo, bali omba kadri uwezavyo na kwa juhudi, pia ni vizuri kuomba maombi ya muda mrefu ya imani.

12.  Wakati mwingine MUNGU hujibu maombi yetu kabla hatuja yaomba.

 Isaya 65:24 "Na itakuwa ya kwamba kabla hawajaomba, nitajibu na wakiwa katika kunena, nitasikia,." 
Ndugu mshukuru MUNGU siku zote za maisha yako maana mambo mengi sana uliyoyahitaji ulijibiwa hata kabla hujaomba, usijivune na kudhani ni akili zako au elimu yako bali ni MUNGU. pia usiacha kuomba hata kama umejibiwa kabla hujaomba.

13. Wakati mwingine MUNGU hukata kuyajibu maombi yetu. 

 2 Wakorintho 12:8-9 "Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi BWANA mara tatu kinitoke, naye akaniambia neema yangu ya kutosha maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu." 
Mambo mengine MUNGU hatakupa kwa sababu sio yako, au hayakusitahili/ hayakufai au ili umtukuze maishani mwako mwote maana kama atakupa unaweza kuangukia mikononi mwa shetani au kuanguka dhambini.

14. Wakati mwingine MUNGU husema ngoja kidogo.

 Zaburi 37:7 "Ukae kimya mbele za Bwana nawe ungojee kwa saburi usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake wala mtu afanyaye hila." 

Kwa sababu MUNGU anatufahamu hata kuliko tunavyojifahamu wenyewe, hutuandalia jambo lililo jema zaidi , usisikitike kama kuna jambo MUNGU hajalijibu bale wewe endelea na maombi na kumsikiliza ROHO MTAKATIFU, pia unaweza kumuuliza MUNGU kwanini hajajibu ombi lako yawezekana kabisa kabla MUNGU hajakujibu bado anakutengeneza kwanza wewe ili hata jambo hilo litakapokuja uwe tayari.

15. MUNGU ni mwenye uwezo hakuna kilicho kigumu  kwake. 

Waefeso 3:20 "Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu." 
Mpendwa omba na BWANA atakujibu na kukupa ukitakacho.

16. Je MUNGU ameahidi kuyajibu maombi yetu kadiri gani?. 

Wafilipi 4:19 "Na MUNGU wangu atawajazieni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya YESU KRISTO." 
MUNGU atatupatia kila kitu ambacho tutaomba sawa sawa na mapenzi yake.
 
17. Je nitajuaje ninachotaka kuomba?. 

 Warumi 8:26-27 "Kadhalika ROHO naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo lakini ROHO mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya roho ilivyo kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo MUNGU." 
ROHO MTAKATIFU ni muhimu sana katika maisha ya kila mkristo. Ndugu yangu mpe BWANA YESU maisha yako na ROHO MTAKATIFU atakuja ndani yako na kukusaidia katika mengi sana ikiwemo jinsi ya kuomba na nini cha kuomba.

18. Katika hali gani KRISTO amesema tutapata majibu ya maombi yetu?. 

Marko 11:24 "Kwa sababu hiyo nawaambia yo yote myaombayo mkisali aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu." 
BWANA anasema yeyote tutakayoomba kwa imani au kwa kuamini yatakuwa yetu.

19. Tuombe kwa imani.
   '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.-Waebrania 11:6.
Imani ni uhakika wa mambo yajayo, na majibu ya maombi ni mambo yajayo hivyo hayo yajayo hutokea tu kama tuliomba kwa imani. 

20. Tusiombe ili tukipata tu tusivitumie vibaya.
   ‘’Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.’’-Yakobo 4:3

MUNGU akubariki sana.
na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.



                 MUNGU akubariki sana .

                  Ni mimi ndugu yako

                  Peter M Mabula

         Maisha ya Ushindi Ministry.

                   0714252292





Comments