Wajibu wa wanawake waliookoka.

BWANA YESU asifiwe ndugu wote.

Leo ni siku ya wanawake duniani.
Nakuletea ujumbe huu kuhusu wanawake, lakini pia kila mtu anatakiwa kujifunza.

MUNGU anawapenda wanawake kama anavyowapenda wanaume.
Kwa MUNGU hakuna cha mwanaume wala cha mwanamke bali kwa MUNGU kuna wateule waliosafishwa kwa damu ya Mwanaye YESU KRISTO.
Kwa MUNGU kuna watoto wake tu waliomtii yeye bila kujali jinsia zao.

2 Korintho 6:18 ''Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike.''

Andiko hili linatufundisha kwamba MUNGU anatupenda wanadamu wote bila kujali jinsia zetu.
Biblia hapo inaonyesha kwamba kama mwanamke au mwanaume atampa BWANA YESU maisha yake, atakuwa ametengwa mbali na shetani na ataingia katika kundi la watoto wa MUNGU wenye haki sawa mbele zake bila kujali jinsia zao.
 Jambo la muhimu kwa kijana wa kike kama ilivyo kwa kijana wa kiume ni kumpa BWANA YESU maisha yako.
Maombolezo 3:27''Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.''

Mwanamke anaitwa msaidizi wa mwanaume, Lakini napenda kukuambia kwamba msaidizi huyu ni kwa ajili ya kumsaidia mwanaume katika  mambo mbalimbali kwenye familia sio kwamba mwanamke ni mdogo kwa mwanaume ila ni kusaidiana,
Hata mwanaume pia ni msaidizi wa mwanamke na sio kwamba mwanaume ni mdogo kwa mwanamke.
Maana ROHO MTAKATIFU pia Biblia inamuita msaidizi wa kuwasaidia watoto wa MUNGU lakini tambua kwamba ROHO MTAKATIFU ni mkuu kuliko vyote tena ROHO MTAKATIFU ni MUNGU, Hivyo anakukua msaidizi tu kwa lengo la kutusaidia katika udhaifu wetu maana hata kuomba inavyotakiwa hatujui, hivyo bila ROHO MTAKATIFU hakuna awezaye kushinda dhambi na kuwa kamili, mkamilifu mbele za MUNGU.
Hata mwanamke ni msaidizi ila sio mdogo wala mnyonge kwa mwanaume.

WANAWAKE NI JESHI KUBWA.
WANAWAKE WANAWEZA KUMTUMIKIA MUNGU HATA KULIKO WANAUME WAKATI MWINGINE.
Ni heri mwanamke yule anayemtegemea BWANA YESU na amemweka BWANA kuwa tumaini lake.
Yeremia 17:7 '' Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.''

                          WAJIBU WA MWANAMKE ALIYEOKOKA.

1: Kumtii MUNGU na kuwaheshimu viongozi wa   ngazi zote kanisani.( Warumi 13:1-3 ''Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na MUNGU.  Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la MUNGU; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye mamlaka? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; )

2: Kushirikiana na wana kanisa wengine kwa upendo.(Warumi 12:10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; ) 

3: Kumtangaza KRISTO kwa ushuhuda wa maneno na matendo.(2 Kor 6:3 ''Tusiwe kwazo la namna yo yote katika jambo lo lote, ili utumishi wetu usilaumiwe; ).

4: Kushirikiana na wanainjili kote duniani kutangaza ufalme wa KRISTO BWANA wetu.

5: Kutumia silaha zote za MUNGU ili kuweza kumshinda shetani kama Biblia inavyosema(Waefeso 6:10-18 ''Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika BWANA na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
 Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
  Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
  na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
  zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
  Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la MUNGU; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote; )


6: Kuwatii waume zao katika BWANA tu.(Wakolosai 3:18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika BWANA. )

7: Kuvaa mavazi masafi ya kujisitiri (1 Petro 3:1-5''Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za MUNGU.  Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini MUNGU, na kuwatii waume zao. )

8:Kuwalinda waume zao kwa maombi.(Yeremia 31:22'' Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume. ).

            YASIYOTAKIWA  KWA MWANAMKE ALIYEOKOKA.

1: Ushauri mbaya kwa wengine unaoweza kusababisha madhara makubwa.( Ayubu 2:9Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru MUNGU, ukafe. )

2: Maamuzi mabaya yanayoweza kuleta maafa.(Mwanzo 3:6Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. )

3: Vichocheo vya ngono ambayo ndio dhambi inayowakosesha wengi.(Wimbo ulio bora2:7''Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. )


4:Dhambi.(Maombolezo 4:6 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwa Kuliko dhambi ya Sodoma, Uliopinduliwa kama katika dakika moja, Wala mikono haikuwekwa juu yake. )


MUNGU akubariki sana.
Hongereni kina mama kote duniani.
Ni mimi ndugu yako. Peter M Mabula.
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292

Comments