WEZI WAIBA MAMILIONI KANISA LA MHUBIRI MAARUFU DUNIANI


Mchungaji Joel Osteen, kiongozi wa kanisa la Lakewood la nchini Marekani.
Watu wasiofahamika wameiba pesa za michango kiasi cha shilingi dola laki sita (600,000) za Marekani pamoja na hundi katika kanisa la Lakewood la nchini Marekani linaloongozwa na mhubiri maarufu Joel Osteen jumapili iliyopita. Awali wizi huo aukutambuliwa mpaka pale mfanyakazi wa zamu aliyetambuliwa kwa jina la Harris County Sheriff's alipofika kanisani hapo siku ya jumatatu saa mbili na nusu asubuhi na kugundua uvunjifu na upotevu huo.

Kanisa hilo limetaka mtu yeyote aliyehudhuria ibada kanisa hapo siku ya jumapili awe makini na akaunti yake ya benki na endapo atagundua jambo lolote lenya ualakini katika akaunti yake basi atoe taarifa haraka iwezekanavyo. Kanisa hilo limewatoa wasiwasi waumini wake kwamba kitendo hicho kisitafsiriwe kwamba kanisa linavujisha taarifa zao bali sadaka hizo zilikuwa za mchango maalumu uliokusanywa wiki iliyopita.

"Tunafanya kazi na polisi kwa ukaribu kushughulikia tukio lililojitokeza", taarifa ya kanisa ikiwa imenukuliwa hivyo, mchango huo tayari ulikuwa una bima hivyo wanaangalia utaratibu na kampuni ya bima ili warudishiwe fedha zilizoibiwa kwa kanisa. Mchungaji Joel ni kati ya wachungaji ambao wanapitia majaribu ya kusemwa vibaya ikiwa pamoja na watumishi wenzie huku pia akihusishwa kuabudu vitu tofauti na Mungu, kubwa zaidi inadaiwa huwa ataji Yesu mara nyingi kwenye mafundisho yake. Lakini licha ya hayo yote huduma yake imekuwa ikihudhuriwa na watu takribani 45, 000 kila wiki.
Sehemu ya kanisa la Lakewood linavyoonekana kwa ndani, Joel akiwa madhabahuni akifundisha.©Lakewood church.
Chanzo : Charisma.

Comments