YESU NI KILA KITU.

Mwl Nickson Mabena katika huduma. akifundisha.

Je! una kiu!?
YESU KRISTO ni Maji yaliyo hai. Yohana 4:14''
walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.''


Je! una njaa!?
YESU KRISTO ni Chakula cha uzima. Yohana 6:51''Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.''


Je! Unataka matunda!?
YESU KRISTO ni Mzabibu wa Kweli. Yohana 15:1''Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na BABA yangu ndiye mkulima.''


Je! unaumwa!?
YESU KRISTO ni Tabibu wa Karibu. Zaburi 103:3-4''Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote, Aukomboa uhai wako na kaburi, Akutia taji ya fadhili na rehema,''


Je! Ume-elemewa!?
YESU KRISTO ni Pumziko. Mathayo 11:28 ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.''


Je! Una vita!?
YESU KRISTO ni Jemedari wa Vita. Isaya 54:17''
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA. ''


 Hivyo una kila sababu ya kutembea kifua mbele. BWANA YESU  akiwa upande wako, nani aliye Juu yako!?.

Songa mbele na BWANA YESU na kama hujampatia maisha yako mpatie leo na atakuokoa na utakuwa huru mbali na magonjwa na nguvu zote za giza.
<<<<<<Amen, Amen>>>>>

           By Mwl Nickson Mabena.

Comments