AGANO LA TATU LIMEGUNDULIWA


Na Apostle Eliya 0759 166 934


AGANO KUU



YALIYOMO; 1).UTANGULIZI 2).AGANO KUU 3).HITIMISHO



DHUMUNI LA SOMO

- Kugundua Agano kuu kati ya sisi na Mungu



ANDIKO KUU; Ezekieli 37:27 Tena maskani yangu itakuwa pamoja nao,nami nitakuwa Mungu wao,nao watakuwa watu wangu.



1. UTANGULIZI

- Kila Mwanadamu asiyesikia au kusoma au kujua hili Agano kuu amelaaniwa, narudia tena A M E L A A N I W A --- YEREMIA 11:3-4. Mtu yeyote asiyejua hili Agano kuu ALAANIWE, ALAANIWE, TENA ALAANIWE kabisa

- Wengi wanajua kuna maagano mawili, la kale (AK) na Jipya (AJ), lakini sio kweli. Agano lipo moja tu, ndio nimeliita AGANO KUU. Kwamujibu wangu AK naliita MCHAKATO KIVULI na AJ naliita MCHAKATO HALISI.

- Ukweli ni kwamba Mungu ameweka agano na kila kilichoumbwa, kalini sitazungumzia haya maagano, mfano; agano la chumvi, Agano la walawi na Yuda, agano la viumbe, agano la marafiki na agano la Macho, badala yake nitazungumzia Agano moja tu --- Agano kuu.



2. AGANO KUU

- Nimemshangaa sana Mungu baada ya kusoma hili andiko TORATI 29:10-15 Mungu aliweka Agano moja(Horebu) na wanadamu wote, Kuanzia Ibrahimu mpaka Mtanzania wa mwisho, rudia kusoma huo mstari wa 15. Bado Yesu akarudia = YOHANA 17:20. Tofauti iliyopo ni MICHAKATO (Matengenezo) ya kufanya hilo Agano liwe halisi. EBRANIA 9:10



A).AGANO LIPO MOJA TU

- Kama Mungu ameweka Agano na kila kiumbe, itakuwa ni ajabu sana asipokuwa na Agano na Mwanadamu, pia itakuwa ni ajabu sana akiwa na Maagano tofauti-tofauti na wanadamu, ndio maana nasema kuna Agano moja.

- Yeremia 11:4. Ahadi Kkuu ya Agano kuu ni Uzima wa milele = 1YOH 2:25

  1. Agano Kuu Moja ni Lipi?  EZEKIELI 37:27

-        Agano kuu hili hapa, Mungu anasema; Maskani yangu itakuwa pamoja nao, Nitakuwa Mungu wao, watakuwa watu wangu. Hili ndilo Agano Kuu, lina sentesi tatu (3) tu.

AU

-        Kwa Kiswahili kingine Mungu angesema; Nitakuwa na mahusiano nae, Nami nitakuwa Mume wake, naye atakuwa mke wangu =ISAY 54:5-6

AU

-        Ni sawa na Mungu kusema; Makao yangu pamoja nao, Nitakuwa Baba yao, Watakuwa wana wangu. = UFUNUO 21:7



-        Sasa ili hili Agano Kuu litimie, kulikuwa na vikwazo ambavyo vilitakiwa viondolewe kwa michakato maalum, hii michakato ndio watu wakaiita Agano la Kale na Agano Jipya. Hii ni michakato tu na sio maagano. YEREMIA 31:33-34



  1. Vikwazo Vikuu cha Agano Kuu.

- Kwazo la kwanza ni Dhambi

    • Dhambi ya ulimwengu YOHANA 1:29
    • Dhambi halisi YOHANA 5:14, 8:11, 1YOH 2:2



- Kwazo la pili ni Mungu na Agano lake kueleweka kwa wanadamu. Sio rahisi mtu amuelewe Mungu asiyeonekana na Agano lake lisiloonekana. Ndio maana Mungu amekuwa akitumia Ahadi, angalau tu aeleweke.   ISAYA 53:1



  1. Vichakatuo Vya Agano Kuu

- Vichatuo ni vitu ambavyo vilitakiwa vifanywe ili Agano kuu lifanyike kisha liwe endelevu;

·        Mungu anaanzisha Agano kwa kutamka NENO MWANZO 12:1

·        Mwanadamu anaitikia kwa kuamini kwa hiyari- TORATI 30:14

·        Mungu anafuta Dhambi za Mwanadamu -- kwa Damu WAEBR 9:12

·        Mungu anampongeza Mtu kwa kuamini anampa Roho - MDO 2:28

·        Mtu anatakiwa atunze Agano -- asimhuzunishe Roho - EFE 4:30



  1. Vielezi vya Agano Kuu

- Ili Mungu aeleweke kwa Mwanadamu, anaambatanisha Ahadi na viapo kwenye Agano kuu, kwasababu sentesi 3 za Agano hazimshawishi Mwanadamu kujibidiisha kwenye Agano kuu;

·        Nchi Mpya 17:7-8

·        Uzazi mwingi MWANZO 28:14

·        Baraka/utajiri/kutawala MWANZO 22:17-18



  1. Ishara(Viashiria) Vya Agano Kuu.

- Kama umegundua ni kwamba Agano ni NENO tu linalotamkwa, hivyo Agano huwa halionekani, kwasababu hiyo Mungu ameweka Ishara ili iwakumbushe wote wawili kuwa wapo kwenye Agano Kuu;

·        Damu --- ni kwa ajili ya Mungu KUTOKA 12:13

·        Kupigwa muhuri --- Nikwa ajili ya Mwanadamu MWANZO 17:11

    =►Malupu-lupu ya Agano Kuu ni Baraka utajiri na kumtawala Adui.



B) MCHAKATO KIVULI NA MCHAKATO HALISI



- Hili Agano la Kale lilitoka wapi ? Hili lilikuwa ni wazo zuri la watu(Baada ya Yesu) kuwafanya watu waelewe utofauti wa kabla na baada ya Yesu, hivyo wakaamua nyakati za kale waziite Agano la Kale na Nyakati za Yesu waziite Agano Jipya. Lakini kiuhalisia, sio maagano.



- Nimekwisha kueleza hapo juu kwamba Agano kuu ni moja lakini michakato ya kufanikisha hilo Agano Kuu ni tofauti kwa uhalisia wake, sasa angalia jedwali hapa chini uone tofauti ya mchakato kivuli na mchakato halisi. Kumbuka Agano Kuu ni Moja




MCHAKATO
KIVULI
HALISI
Nchi Tarajiwa----
Kanaani =LAW 25:38-------------
Mbingu Mpya=UFUN 21:1
 Makuhani---
Walawi = HESABU 17:8
Yesu = WAEBR 5:6
Wafalme-----
Yuda =
Yesu = UFUNUO 17:14
Kafara------
Wanyama = LAWI 23:19
Yesu = WAEBRANIA 10:10
Dhambi------
Kusitiriwa = ZABURI 85:2
Kufutwa = EFESO 1:7
Viongozi----
Torat/makuhani=
Roho Mt =RUMI 8:9
Msamaha-----
Kila sabato= EBR 10:11
Mara moja tu= EBRA 9:12
Sheria------
Zaidi ya 600
1 = EFESO 4:30
Amri
10 = KUTOKA 34:28
2 =MATHAYO 22:37-40
Dalili za Uwepo-------
Sanduku = KUTOK 29:43-46
Roho Mt = EFESO 1:13-14
Vita na adui
Mataifa = TORAT 20:17
Shetani/pepo =EFESO 6:16
Wahusika wakuu-------
Israeli tu =KUTOK 3:10
Mtu yeyote =MARKO 16:15
Tohara------
Zunga = MWANZO 17:11
Moyo =YEREMIA 4:4
Makutanio----
Sandukuni =KUTOK 25:22
Moyoni = KOLOSAI 1:27
Kuhesabiwa haki---------
Kwa Sheria =LUKA 1:6
Imani =RUMI 1:17
Ghafi za Hekalu-------
Jengo =1FALME 5:18
Mwili =1 KORINTHO 3:16
Makao ya Roho
Nnje,juu = ISAYA 61:1
Ndani = YOHANA 14:17
Thawabu------
Ya muda = EBRANIA 4:8
Uzima milele = MDO 13:48







    

C) MCHAKATO KIVULI



- Agano Kuu lilianzia kabla ya ulimwengu kuumbwa = TITO 1:2, Adam na Eva, wakalivunja, Mungu akawafukuza. Toka hapo Mungu akaanza kutafuta mtu atakayekubali kufanya nae Agano tena, lakini huyo mtu shariti asiwe na dhambi, kwahiyo mahangaiko yoote ya watu wa kale ni kuondoa kikwazo cha Dhambi, lakini haikuwa rahisi kuondoa dhambi kama walivyodhani. MWANZO 3:24



- Mara zote Mungu amekuwa akimtaja Ibrahim, Isaka na Yakobo katika Agano kuu WAAMUZI 2:20, Kwasababu ya kutii kwao aliwapa na AhadiUzao, Nchi na Baraka = MWANZO 17:14. Pia akaweka Ishara ya Agano naoKutahiliwa, yote hayo hayakuwa Agano = JOSHUA 5:2. Ninashawishika kuona kwamba Mungu anajua vizuri sana namna ya kuuza wazo lake la Agano.



- Chunguza hizi sehemu tatu 1) Misri 2)Horebu(Jangwani) na 3) Kanaani. Mungu aliwakomboa Israeli Misri ili aweke nao Agano = KUTOKA 8:1, akaweka nao Agano Jangwani(Horebu)= TORAT 5:2, ili akaishi nao Kanaani=WALAWI 25:38. Zoezi hili halikuwa rahisi. Mungu kupata hisia zao aliamua atumie utumwa wao kuwatajia Nchi yenye Maziwa na Asali, jangwani ilikuwa ni shule ya kuishi kanaani= TORATI 4:10.



- Kama wewe ni msomaji mzuri wa Biblia utakubaliana na mimi kwamba kila kitu kilichokuwa kikitumika kwa ajili ya Mungu wakati wa kabla ya Yesu kiliitwa -- cha Agano. Ikumbukwe kuwa vyenyewe SIO Agano ila ni vitu vya Agano;

·        Sanduku la Agano = 2 NYAKATI 5:7

·        Torati ya Agano = 2 WAFALME 23:2-3

·        Damu ya Agano = KUTOKA 24:8, MATHAYO 26:27-28

·        Ukuhani wa Agano = MALAKI 2:4-5

·        Mbao za Agano = TORATI 9:9

·        Waisraeli-Taifa la Agano = 2 SAMWELI 7:23-24



Sina uhakika sana kama Israeli walikuwa wanajua wanachokifanya, ni kanakwamba Mungu alikuwa anawalazimisha ingawa ni kwafaida yao wenyewe. Nina uhakika, Zoezi la ibada, Sheria, Vita nk vilikuwa vinawakela sana = 2FALME 17:15, kwasababu walikuwa hawajui dhumuni, lakini wachache walitambua. Swali; Watu wangapi walitoka misri na wangapi walioingia Kanaani ?



-Ndivyo Mungu alivyofanya kwetu, ametutoa mikononi mwa 1)Shetani=KOLOSAI 1:13 ili tufanye nae Agano kwa 2) Yesu na Roho(Duniani)=ISAYA 53:11b ili tukaishi na Mungu 3) kwenye Ufalme wake = MATHAYO 8:11. Tupo hapa Duniani kujifunza namna ya kuishi mbinguni, pia wengi wetu hawajui dhumuni, hivyo wengi hawataingia kwenye Ufalme = MATHAYO 7:14. Lakini ashukuriwe Mungu kwani watu wengi miaka hii wameanza kuelewa.= UFUNUO 5:9



D) MCHAKATO HALISI YESU

- Utagundua mvunja Agano siku zote ni Mwanadamu, labda waisraeli hawakujua umuhimu au walifanya makusudi au walijua umuhimu lakini hawakuwezeshwa, vyovyote vile, Mungu aliamua atatue matatizo yote ya Agano Kuu kwa kumleta Mwanawe Yesu = KOL 1:20.Kipi kilimfanya Yesu aje?



1. Dhumuni la Ujio wa Yesu;

·        Kubadiri kivuli kuwa Halisi = WAEBRANIA 8:13

·        Kusajiri watakaoingia kwenye Agano Kuu = UFUN 5:9-10



2 Yesu na Tarajio Jipya.

- Yesu alikuja kutoka mbinguni, anapotaja ulimwengu ujao anauhakika.

·        Ufalme wa Mungu = YOHANA 14:2-3

·        Uzima wa milele = TITO 1:2

·        Kutawala milele = UFUNUO 22:5



3. Vikwazo vya Agano kuu kwa mujibu wa Yesu.

- Kikwazo hapa sio dhambi, kikwazo kimebadirika

·        Kutomwamini Yesu = YOHANA 8:24

·        Kumkufuru na kumhuzunisha Roho Mt = MATH 12:31, EFESO 4:30



4. Vichakatuo vya Agano Kuu kwa mujibu wa Yesu

- Mambo yanayowezesha kuwepo kwa Agano Kuu kwa mchakato Halisi

·        Yesu (Injili)= 1 KORINTHO 15:1-4

·        Roho Mt = RUMI 8:14

·        Mwamini = 1 WATHESALONIKE 5:10

Tunayapokea Yote haya kwa kuliamini jina la Yesu = WARUMIN 10:9



5.Ishara za Agano Kuu kwa mujibu wa Yesu

- Sifa ya Ishara au kiashiria ni lazima kionekane, sasa utamjuaje mtu aliye ndani ya Agano Kuu ?

·        Kumwamini Yesu = YOHANA 11:25

·        Uwepo wa Roho Mt- Karama na Matunda = 1 KORINTHO 12:4-6

·        Kuwa na Nguvu- Kutoa Mapepo = LUKA 11:20, 1 KORI 4:20

   =Ahadi kuu ya Agano kuu ni uzima wa milele = yuda 1:21



E) MUNGU KUTIMIZA AGANO LAKE KUU

- Baada ya Mambo yote, na michakato yote kutimizwa ndio sasa Mungu anasema nitalitimiza Agano langu Kuu. Mungu atafanya makazi na wanadamu,atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake. Itakuwaje ?



1.Kufanywa UpyaKila kitu kitafanywa upya, huwezi amini

·        Mbingu mpya = UFUNUO 21:1

·        Nchi mpya = UFUNUO 21:1

·        Mji mpya = UFUNUO 21:2

·        Utu mpya = KOLOSAI 3:10

Soma hapa uone Mungu anavyosema; UFUNUO 21:7



2. Hatimaye Agano Kuu kutimia

- Yote yakisha fanywa upya, sasa ndio Mungu atalitimiza Agano lake Kuu rasmi. Unakumbuka sentesi tatu(3) za Agano letu na Mungu ?

·        Maskani ya Mungu ni pamoja na Wanadamu = UFUNUO 21:3

·        Atakuwa Mungu wa Wanadamu na = YEREMIA 32:27

·        Wanadamu watakuwa watu wa Mungu = HOSEA 2:23



3. HITIMISHO

- Muda huu tunaoishi hapa Duniani ni sawa na Wana wa Israeli walipokuwa Jangwani, usitegemee Mungu kukufanikisha yote unayoyataka ukiwa hapa Duniani, sio kwamba hawezi au hujamuomba, la hasha, anataka utamani kwenda kwenu. Ukitakakuelewa soma hadithi ya Israeli jangwani. =EBR 13:14



- Agano Kuu lipo moja, hakuna Agano la Kale wala Agano Jipya, hivyo leo piga magoti umwambie Mungu kuwa unataka kuingia Agano naye;

Awe Mungu wako, Uwe mtu wake, na siku ya mwisho, Patakatifu pake pawe katikati yako na watakatifu wote.  


By Apostle Eliya 0759 166 934

………..Remember……………THE BEST HAS COMES…………………..

Comments