![]() |
Rais Dr Jakaya Kikwete |
![]() |
Viuongozi wa UKAWA |
Askofu Dr Boaz Sollo akiwa katika moja kati ya mikutano yake ya kuliombea Taifa amani
UMOJA wa katiba ya wananchi (UKAWA) wazidi kukaliwa kooni baada yaaskofu wa kanisa la Overcomers Power Centre Iringa Dr Boaz Sollo kupinga vikali uamuzi wa UKAWA kutoka bungeni na kwenda kwa wananchi kabla ya kuifanya kazi waliyotumwa bungeni kama wajumbe wa bunge la katiba na hivyo kumshauri Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Kikwete kulivunja bunge hilo ili kuepusha amani kuvurugwa nchini.
Huku
akisema kuwa akiwa kama mtumishi wa Mungu anaamini kabisa kuwa
serikali mbili ni jibu la watanzania katika endeleza umoja ,amani na
mshikamano ulioachwa na waasisi wa Taifa hili hayati Baba wa TaifaMwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume Rais waKwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendelea kuvurungwa na wanasiasa wachache wasiopenda amani ya nchi hii .
Akizungumza na
mtandao huu wa www.matukiodaima.com kwa njia ya simu kutoka jijini Dar
es salaam ambako amealikwa kwa huduma za kanisa , askofu Dr Solloa
alisema kuwa tayari kanisa lake limeanza kufunga na kuomba kwa ajili
ya amani nchini na kuliombea bunge hilo la katiba ili mwenyezi
Mungu kuliunganisha bunge hilo na kuepusha mgawanyiko ulioanza
kujitokeza na kundi hilo la wana Siasa wanaojiita wana UKAWA .
"
Watamzania tulipongeza uteuzi wa Rais wetu mpendwa Dr Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kuteua miongoni mwa watanzania wachache kati ya wengi
kwa ajili ya kwenda kushiriki bunge hilo kuandaa katiba ya nchi huku
tukiamini kuwa walioteuliwa wangetufikisha pazuri zaidi tofauti na
ilivyo sasa ambapo wajumbe hao wameanza kuhatarisha amani na utulivu
nchini "
Kitendo
cha wajumbe wa bunge hilo kutoka nje ya ukumbi na kutaka kuanza
kuzunguka mikoani ni sawa na kuwasaliti wananchi ambao walikuwa
wakisubiri kwa hamu wajumbe hao kuwaletea katiba mpya ila sasa wameanza
kutishia amani ya nchi kwa kutafuta huruma ya wananchi katika kuungwa
mkono wao na vyama vyao.
" Ushauri
wangu kwa mheshimiwa Rais Dr Kikwete ni kulivunja kabisa bunge hilo
ili kunusuru amani ya nchi hii ambavyo dalili ya kuvurugwa imeanza
kujitokeza kupitia UKAWA ....tulitegemea wajumbe hao wangebaki ndani ya
bunge na kutuandalia katiba bila kuunda umoja wa kuanzisha vurugu
nchini kwani wote bila kujali vyama vyao na taasisi zao walizotoka
walipaswa kuwa kitu kimoja katika bunge hilo kwa kuwasilisha hoja za
kuwa na katiba bora si vinginevyo "
Alisema
kuwa ni vema kuendelea na katiba iliyopo kuliko kusubiri katiba ya
wajumbe hao ambayo mwelekeo wake si mzuri bali upo kwa ajili ya
matakwa ya wachache kisiasa .
Askofu
huyo alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wanachanganywa na wana siasa
hao ila ukweli wazanzibar na watanzania wanapenda kuona amani
iliyopo inaendelea kuwepo na suala la maendeleo linaendelea na sio
utitiri wa serikali hali maisha yao kiuchumi ni duni .
Hata
hivyo alisema kutokana na mwenendo wa bunge hilo kwa sasa kanisa
lake limetangaza mfungo wa maombi maalum kwa ajili ya Tanzania ili
kuepuka chuki kupandikizwa na wachache kwa lengo la kuvuruga amani yetu
.
Comments