![]() |
Ailyekuwa mkurugenzi wa WWI Taifa, EAGT - Mama Benja, enzi za uhai wake. |
Taarifa za kusikitisha ambazo zimetufikia hivi punde ni kwamba
mkurugenzi taifa wa wanawake wa injili wa kanisa la Evangelistic
Assemblies of God Tanzania anayefahamika kwa jina la Mama Benja,
amefariki dunia.
Kwa mujibu wa familia, hadi mauti yanamkuta Mama Benja, presha ilikuwa
chini kiasi cha kulazwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya. Taarifa
zaidi zinaeleza kuwa maazishi yatafanyika siku ya Jumanne mkoani Mbeya.
Miaka ya 1974 huko Bugando mjini Mwanza ndipo historia ya Mama huyu
imetambuliwa kuanzia, ambapo alikuwa mmoja wa viongozi wa WWK enzi hizo kanisa la Bugando (alikoanzia marehemu Askofu Moses Kulola)
likiwa chini ya TAG, wakati huo pia mume wake akiwa mzee wa kanisa.
Miaka 6 iliyopita alikuwa makamu wa WWI EAGT na hatimaye 2011 kuwa
Mkurugenzi kamili.
Licha ya kuwa muinjilisti wa muda mrefu zaidi, shujaa huyu wa injili
kwa zaidi ya miaka 30 amekuwa pia kiongozi wa wamama kwa kipindi kirefu akishika nyadhifa mbalimbali.
Tutaendelea kukufahamisha zaidi kwa kadri taarifa zitakavyokuwa
zikitufikia, kaa na GK. BWANA ametoa, na BWANA ametwaa, jina la BWANA
lihimidiwe.
Marehemu mama Benja kwenye maazishi ya aliyekuwa makamu mkurugenzi wa Wanawake wa Injili taifa, Mama Nyanda.Chanzo:Gospel Kitaa |
Comments