FILAMU YA YESU SASA MTAANI KATIKA MFUMO MPYA KUANZIA APRIL 1



Kwa wale wadau wa filamu, hasa katika mfumo wa blu ray, hatimaye ili filamu iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kutoka kwake upya, The Jesus Film, sasa imeingia mtaani leo hii. Filamu hii ambayo ndio inayoongozwa kutazamwa kwa filamu za Kikristo zilizowahi kutengenezwa, haiishii hapo, filamu ya Jesus pia ndio inayoongoza kwa kutafsiriwa katika lugha nyingi zaidi ulimwenguni.

Na ni filamu hii hii ambayo imetengenezwa miaka ya sitini, kuonesha maisha ya Yesu yalivyokuwa kwa mujibu wa Biblia, ambapo baadhi ya watu hudhani ya kwamba ni Yesu mwenyewe anayeokana, ilhali akiwa ni muigizaji Bryan Deacon.

Hatua ya DVD ya filamu ya The Jesus Film kuingia mtaani leo hii, ni jambo ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu, ambapo mfumo mzima wa filamu hiyo umerekebishwa, kwa habari ya sauti, picha zake na hata upande wa rangi. Kama umewahi kuiona filamu hii, basi ni vema pia ukaisaka katika mfumo huu an'gavu ama HD ujionee tofauti ya kipindi hicho, na hivi sasa, ambapo filamu hiyo bado inafanyika baraka na kukuza ufalme wa Mungu.

                          Chanzo ni Gospel kitaa

Comments