Leo tarehe 26 April muungano wa Tanganyika na Zanzibar umetimiza miaka 50. Tunamshukuru MUNGU kwa hatua hii njema . Maombi yangu amani iendelee siku zote na Bunge la katiba wafanye maamuzi mazuri ya kuwapendeza watanzania wote.
Hongera Tanzania.
Hongera nchi yangu.
MUNGU ibariki Tanzania.
MUNGU wabariki watanzania wote.
Katika jina la YESU KRISTO amen.
 
 
 
 
Waasisi
 wa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar, Hayati Baba wa 
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na Hayati,  Abeid Aman 
Karume (kulia waliokaa) wakisaini nyaraka za Muungano mwaka 1964. 
Mwalimu
 Julius Kambarage Nyerere akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar,
 huku akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar, Abeid Aman Karume, (wa tatu 
kushoto) na Mhe. Rashind Mfaume Kawawa (wa kwanza kulia) wakati wa 
sherehe za kwanza za Muungano zilizofanyika Tarehe 26 Aprili, 1964. 
Mwalimu
 Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na  Sheikh Abeid Amani Karume 
(kulia) wakibadilishana Hati za Muungano wa Tanganyika na  Zanzibar 
Aprili, 1964. 
Waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (kushoto) na Hayati Abeid Aman Karume. 
 
 
Comments