IGIZO LA YESU 'PASSION OF CHRIST' KUPAMBA IJUMAA KUU JIJINI LONDON KESHO

Ijumaa ya kesho itakuwa wakati mwingine kwa wakazi wa jijini London nchini Uingereza, na watembeleaji wa jiji hilo ambao watabahatika kufika eneo la wazi la Trafalgar square lililopo katikati ya jiji hilo kupata fursa ya kujionea kwa mara nyingine igizo la maisha ya Yesu ambalo hufanyika kila mwaka siku ya Ijumaa kuu katika eneo hilo kuanzia majira ya saa sita mchana bila ya kiingilio.

Mwigizaji mkuu katika igizo hilo anafahamika kwa jina la James ambaye muonekano wake anafanana kabisa na mwigizaji wa filamu ya Yesu ama Jesus Film bwana Brian Deacon. Igizo hilo litaanza majira ya saa sita mchana ambapo taasisi inayoandaa onyesho hilo linalofahamika kama 'Passion of Christ' hufanya igizo hilo mara mbili saa sita na saa tisa alasiri.




Kuangalia picha zaidi katika onyesho la mwaka jana BONYEZA HAPA.

Comments