JE UJANA WETU KAMA TULIOOKOKA NI KIELELEZO?

Kijana ni mtu wa kike au wa kiume
mwenye umri kati ya miaka 15 na 45.
Biblia inasema nini juu ya kijana?
Biblia imenena mambo mengi juu ya
kijana, na baadhi ya hayo ni kuwa
fahari ya kijana ipo katika nguvu
zake (Mithali 20:29-
Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi. ). 

Kijana ana
nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa
ndani yake na kisha amemshinda
shetani(1Yohana 2:14b-17
Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu. Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. ).


BWANA YESU asifiwe.

Licha ya kuwa na nguvu nyingi, je ujana wetu ni kielelezo?

"1TIMOTHEO 4:11-13- Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha. Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. Usiache kuitumia karama ile iliyomo ndani yako, uliyopewa kwa unabii na kwa kuwekewa mikono ya wazee. ''

BIBLIA inaeleza baadhi ya mambo ambayo yanamfanya kijana aliyeokoka kuwa kielelezo kwa waaminio na yamkini wasio amini pia, mambo hayo ni kama ifuatavyo kama tulivyosoma hapo juu ktk 1TIMOTHEO 4:11-13. 

(1)USEMI MZURI 

(2)MWENENDO MZURI, 

(3)UPENDO,

 (4)IMANI,

 (5)USAFI/UTAKATIFU, 

Pia kuna mambo mengine 3 ya mhimu ambayo ni KUSOMA, KUONYA na KUFUNDISHA. 

Mwisho anaonyesha kitu kingine cha mhimu katika mstari wa 14 anasema usiache kutumia KARAMA iliyomo ndani yako. 

Kama basi ukitaka kuwa kielelezo lazima uzingatie hayo! 

 Mungu wa mbinguni atusaidie kuyashika hayo sisi kama vijana tuliokoka. 

Barikiwa sana na YEHOVA MUNGU!
By mtumishi Alex.

Comments