JE WEWE UNAWAZA NINI JUU YA BWANA?

INJILI KAMA HII INAWAFIKIA WENGI SANA .

Katika kutekeleza AGIZO KUU la Bwana Yesu, la Kuubiri Injili kwa kila kiumbe, mwezi February mwaka huu, mimi na rafiki zangu wawili tulianza utaratibu wa kuhubiri mitaani kwa kutumia Megaphone.

Ratiba yetu ya kuhubiri ni kila siku ya Jumatano na Ijumaa, saa 12:30 - 02:00 asubuhi, kabla hatujaenda kwenye kazi zetu.


MATOKEO:

1. Watu watano wameshamjia Bwana, wanaendelea vizuri kanisani kwetu.


2. Wengi wamesikia Injili, wapo wengi watakaookoka na kulelewa kwingineko.


3. Kundi letu limeongezeka, tulianza watatu sasa tuko sita.


4. Vipawa vya Uinjilisti vimeonekana na vinakua.


5. Kiu ya kumtumikia Bwana inaongezeka kwangu na kwa wenzangu.


MALENGO:

1.Kuhubiri kwa kutumia Spika kubwa inayosukumwa kwenye ki-troli kabla haujafika mwezi Julai.


2. Wakati waja tutakapohubiri kwa kutumia HIACE, spika zikiwa zimefungwa juu!


3. Mkazi wa Mbagala, atakayetupwa Jehanamu, iwe ni kwa kutaka kwake!


Tutahakikisha kila sikio linasikia Habari Njema za Mwokozi Yesu!

WEWE UNAWAZA NINI JUU YA BWANA?

MUNGU wa mbinguni akubariki sana .
By Alex Emmanuel Bubelwa.

Comments