KANISA LA TANGU MKOLONI LINA MIAKA 82 - MOSHI


Kanisa hili lilijengwa tarehe 17/10/1932 ma mkoloni mkoani Arusha na kupewa jina la TEREVEN maana yake "Ombeni" kwa Kiebrania ni "Rogate" . Kanisa hili lipo katika Usharika wa Lyamungo jimbo la Kaskazi huko Moshi.
Kanisa hili kwa sasa halitumiki lakini bado liko imara sana. Askofu Martin Shayo wa kanisa hilo amesema kwa sasa hawatumi hilo kanisa na badala yake wamehamia katika kanisa jipya ambalo bado halijakamilika.

Siku ya  ibada ya J/pili kulifanyika harambee ya kukusanya pesa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa ambapo mgeni rasmi alikuwa YESU mwenyewe ambapo muendesha shughulia MC Heavenlight Massawe alichukua kiti na kukiweka mbele ya madhabahu na kutamka leo katika harambee hii hatuna mgeni rasmi hivyo mgeni rasmi yuko hapa mbele ni YESU mwenyewe hivyo na mkaribisha akae na kisha akaendelea na kazi yake.





Kanisa jipya likiwa bado kwenye matengenezo.




Kwaya ikiimba.

Kanisa jipya lilianza kujengwa mwaka 2009 linatarajiwa kumalizika mwaka 2017 Mungu akipenda...kanisa hilo jipya linakadiriwa kuchukua watu 2500 kwa wakati mmoja.

Kushoto ni Mwenyekiti wa jengo mzee Matinga akiteta jambo na mzee wa kanisa.



Mc akiendelea na harambee



Ukimuangalia MC mbele yake kuna kiti.....hicho kiti ndicho alichopewa mgeni rasmi "YESU" mpaka ripota wangu Everlight anatoka mahali hapo kulipatikana pesa milioni 12.

Source: Uncle Jimmy

Comments