KUILIMA NA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI * sehemu ya pili *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Blessed be the name of the Lord....
Say;
AMEN.
Jina la Bwana Yesu lisifiwe...

Leo ni siku ya pili ya fundisho hili,ambapo tunakwenda kujifunza kwa ufupi,lakini kumbuka;
Nilikuambia ya kwamba EDENI haikuwa bustani ya kawaida wala EDENI haikupandwa,kama bustani nyingine zipandazwo,Bali EDENI ilikuwa ikiwakilisha UWEPO wa Mungu.

Maana maandiko matakatifu yametuelezea vizuri kabisa ya kwamba Edeni ilikuwapo tu,Bali ndani yake BWANA Mungu ndimo alipopanda bustani,hivyo bustani hii ikaitwa bustani ya Edeni sababu ilikuwa ikipatikana ndani ya edeni (Mwanzo 2:8)

Haleluya...

BWANA Mungu akamuweka mtu ndani ya Edeni ailime na kuitunza.
Kwa lugha nyingine,Mungu alimuweka mtu ndani ya Edeni AFANYE KAZI.Huyu mtu aliyewekwa ndani ya Edeni,aliwekwa ndani ya uwepo wa Mungu ili AFANYE KAZI,AFANYE KAZI NDANI YA UWEPO WA MUNGU. Kazi yenyewe ni kulima na kutunza.
Hivyo basi,mtu amewekwa ndani ya uwepo wa ki-Mungu kwa makusudi mawili tu;
01.Kulima.
02.Kutunza.

Kila mwanadamu chini ya jua ameumbwa kwa makusudi na maana kamili.Hakuna mwanadamu aliyekuja kwa bahati mbaya.Pia hakuna mwanadamu aliyeumbwa pasipo kupewa kazi ya kufanya.Wewe pia umepewa kazi ya kufanya,kazi hiyo uliyopewa ni KUILIMA NA KUTUNZA EDENI.

" BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu,akamweka katika bustani ya Edeni,ailime na kuitunza." Mwanzo 2:15

Mtu aliumbwa ili akafanye kazi ndani ya Edeni,kwa lugha nyepesi ;
mwanadamu aliumbwa akayafanye mapenzi yake Baba Mungu muumba wa vyote.Ndio maana unaona pale alipoumbwa mtu akaeekwa ALIME na KUTUNZA.
Kulima ni kufanya kazi.

BWANA Yesu asifiwe...

Kuilima bustani ya Edeni ni nini?
JIBU:
Kuilima bustani ya Edeni ni kufanya kazi katika shamba la BWANA Mungu.
Adamu alipewa kila kitu ndani ya bustani,lakini haikutosha mbele za Mungu,maana alihitajika ALIME.
Alihitajika afanye kazi ndani ya shamba la BWANA Mungu.

Uwepo wa Mungu ambao mwanadamu amewekwa ndani yake,ni pale BWANA Mungu alipomuumba mtu na kumuweka ndani ya Edeni.
Adamu alikuwa uweponi mwa BWANA Mungu ndio maana chochote alichokisema Adamu kilikuwa ni ndio mbele za BWANA Mungu.

"BWANA Mungu akamfanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni,na kila ndege wa angani,akamletea Adamu ili aone atawaitaje;kila kiumbe hai,jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake." Mwanzo 2:19

Biblia inasema Adamu alipoletewa wanyama,kila jina aliloliita likawa ndio machoni pa BWANA Mungu,hii inamaanisha Adamu alikuwa uweponi kiasi kwamba chochote alichokiita kilikubaliwa na BWANA Mungu.Tazama hata wakati mwingine BWANA Mungu alikua akishuka wakati wa jua kupunga kusudi wazungumze na Adamu,(Mwanzo 3:8)

Kwa lugha nyinge ni
kwamba kulikuwa na muunganiko/USHIRIKA WA ROHO MTAKATIFU baina ya BWANA Mungu na Adamu.

Hivyo mtu huyu,alipoumbwa akawekwa ndani ya uwepo wa Mungu kwa kusudi maalumu la KUFANYA KAZI.
Ndani ya UWEPO wa Bwana Mungu,ipo kazi ya kufanya,haijalishi kwamba kuna kila kitu kilichowekwa tayari kwa ajili yetu.

Kulikuwa na kila kitu kilichowekwa tayari kwa mtu aliyeumbwa na BWANA Mungu ndani ya Edeni/UWEPONI.Ile namna ya kuwa na kila kitu ndani ya UWEPO WA KIMUNGU haimaanishi tukae na kubweteka,Bali tumewekwa kwa ajili ya kufanya kazi.

Kuwekwa ndani ya UWEPO wa Mungu kwa njia ya kuokoka ni Neema,Lakini utakatifu ndani ya UWEPO ni wa KUULIMA,yaani ni wa kutafuta.Kamwe utakatifu hauji kwa kukaa pasipo kuutafuta maana utakatifu sio kwa neema.Ndio maana mtu alipoumbwa akajikuta tu amewekwa ndani ya Edeni lakini ndani ya Edeni akaambiwa afanye kazi.

Leo hii,watu wote waliookolewa,wameokolewa kwa neema tu,lakini ndani ya wokovu BWANA Mungu anasema leo KUUFANYIA KAZI pamoja na KUUTUNZA WOKOVU KWA GHARAMA YOYOTE ILE,HATA KUFA NA TUFE.
Shamba la Bwana li hai,lakini ni wewe unaehitajika kulilima na kulitunza.

Leo tunaanza lasmi kujifunza namna ya kulima ndani ya Edeni.Maana inatubidi kujifunza ulimaji,kisha tukimaliza tutajifunza namna ya kutunza Edeni.

Haleluya...
Ooh,Groly to God...

01.KUILIMA EDENI.
Wakulima siku zote huwa hawachoki kulima hata wakati wa kiangazi,utawaona muda wote wakipanda mbegu kisha wakimuagilia kwa mkono huku wakiamini kwamba mbegu walizopanda zitaota tu.Na hiyo ndio kanuni moja wapo ya mkulima wa kawaida kabisa.

Tunapoangalia upande wa pili wa maisha yetu ya imani,nasi ni lazima kuilima Edeni sababu ndio kazi tuliyopewa na BWANA Mungu.Pasipo kuangalia ni matunda gani tutavuna.

Haleluya...

Uliokolewa kwa neema,kisha ukawekwa mahali fulani kuukulia wokovu,mahali hapo pia ni shamba la BWANA Mungu.Ipo kazi ya kufanya mahali hapo ulipo,maana hapo ulipo hukukaa kwa shauri lako Bali shauri la BWANA Mungu.Adamu hakuwekwa katika Edeni kwa shauri lake,Bali Mungu ndie alipomuona akaonelea amuweke katika Edeni kwa shauli la Mungu.

Watu wengi hawafanikiwi sababu wamekataa kufanya kazi ya Bwana mahali walipo.Ninaposema wamekataa simaanishi kwamba wamekwisha tamkaa kwa midomo yao kwamba " ...hatufanyi..."
Bali wamekataa kwa kutokutii neno la BWANA Mungu linalopitia kinywa cha mtumishi wake aliyemuweka akuchunge wewe.

Biblia inatupa msingi mkubwa sana wa kufanikiwa katika maisha yetu ya kiroho na ya kimwili pia,msingi huo ni kufanya kazi/kufanya mapenzi yake Baba wa mbinguni kwa kulisikia neno na kuwa mtendaji wa neno.

Kulima ni jukumu lako pia,wala sio jukumu la wachungaji peke yao.Kanisa unaloabudu ni shamba la Bwana.Shamba hilo linahitaji mtu wa kulima,na mtu anayehitajika ni wewe.
Hatukuitwa tukaye nyumbani mwa BWANA kwa hasara pasipo kufanya kazi.
Leo hii watu wamekaa tu,pasipo kufanya kazi huku mioyoni mwao wakijihesabia haki wakijiita " wateule ".

Kanisa limeshindwa kusonga mbele ipasavyo kwa sababu wapo watu waliokoka wasiotaka kufanya kazi.
Mfano;
Mara nyingi watu hufanya kazi za kanisa mpaka wasukumwe na mchungaji,utakuta vyoo ni vichafu,sasa mpaka aje mchungaji au kiongozi ndio aanze kusukuma watu wakasafishe.

Mara nyingine utakuta mtu akichelewa kuja katika nyumba ya Bwana siku ya ibada pasipo sababu yoyote ile.Na mtu wa namna hii wala hajisikii kuumia moyoni mwake.Jamani !Hukuwekwa hapo kanisani ujiendeshe utakavyo wewe,Bali yakupasa uendeshwe na BWANA Mungu aliyekuweka.

Haleluya...

Edeni ya BWANA inahitajika kulimwa.
Bwana Mungu hajakuokoa ili uende mbinguni tu,Bali umeokoka ili ufanye kazi ya BWANA Mungu na atimaye uende mbinguni,wokovu wako ni kulima Edeni siku zote.

Swali;
Unalimaje?

JIBU;
Ili uweze kulima ni lazima uwe na vitendea kazi,mfano uwe na jembe,uwe na ardhi ya kulimia n.k
*Ardhi ni maeneo yoyote uliyopangiwa na BWANA Mungu.
*Vitendea kazi,ni JINA LA YESU KRISTO PEKEE,na wala si majina mengine,eti kwamba utumie majina ya mitume kwa kufanya kazi ya Bwana!Kamwe hayatumiki hayo majina mengine,
Biblia inasema;

" Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote,kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." Matendo 4:12

Jina la Yesu ndilo jina la pekee lililothibitishwa na Mungu mwenyewe,lenye nguvu,mamlaka,utiisho.
marehemu shetani amepofusha fahamu za watu,hata watu wakitumia majina ya mitume waliokufa wakiomba kwa msaada kwa majina hayo,tena wakiomba msaada wa ulinzi kwa jina la mama yake Yesu.
Mimi nakuambia leo usikubali kufanya hivyo tena;shtuka sasa!

Tunalima Edeni kwa kitendea kazi cha jina la BWANA YESU KRISTO tu....

ITAENDELEA....

Usikose muendelezo wa fundisho hili,ambapo sehemu ijayo tataenda kuingia ndani kwa sehemu yake.
Kwa huduma ya maombi na maombezi usisite kunipigia;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Comments