KUILIMA NA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI * sehemu ya mwisho *

"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu,akamweka katika bustani ya Edeni,ailime na kuitunza." Mwanzo 2:15
Bwana Yesu asifiwe....
Haleluya...
Haleluya...

Yapo maagizo na kanuni ndani ya EDENI.Mtu alipowekwa ndani ya bustani ya Edeni alipewa agizo hili;
Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
" BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,
walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika. " Mwanzo 2:16-17
Tamko hilo lilielekezwa kwa mtu ambaye Bwana Mungu amemfanya. Na lipo wazi kabisa ya kwamba huyo mtu amekatazwa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya,ila anaweza kula matunda yoyote yale.Agizo hilo limefuatiwa na adhabu.
Haleluya...
Nasema Haleluya...

Sikia;
Nyumbani mwa Bwana yapo maagizo aliyoyaagiza BWANA Mungu kupitia watumishi wake aliowaweka.Mfano mtumishi anawaambia waamini tamko/agizo la kula mshahara wao lakini sehemu ndogo ya kumi ya mshahara wao wasile,maana sehemu hiyo ni mali ya BWANA,

Na endapo wakila hakika watakufa,lakini inatokea watu hawa wanakula na hatimaye hufa kiroho na kiuchumi pia ,
sababu ya kutokutii agizo la mtumishi wa Mungu ambaye haneni kwa shauri lake bali la Mungu.

Mfano huo ni mdogo sana kati ya mifano mingi ambayo tunaagizwa na watumishi wa Mungu tena kushindwa kuitii.Kwa mfano huo;yeye aliyekatazwa asile sehemu ya kikumi chake cha mshahara kisha akala ni sawa kabisa na agizo aliloambiwa Adamu ya kwamba aweza kula matunda ya miti yote isipokuwa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Biblia inaendelea kutueleza sababu iliyomfanya Adamu na Hawa kula matunda ya mti waliokatazwa na BWANA Mungu.Tunasoma;
" Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? "Mwanzo 3 :1
Maandiko matakatifu tuliyoyasoma hapo juu yanatueleza jinsi nyoka alivyokuwa mwerevu akimdanganya Hawa.
Sasa emu pata picha hii;
Chukulia upo katika nyumba fulani,kisha mwenye nyumba aliyekuweka katika nyumba yake uitunze akwambie;
" fulani,waweza kuingia katika vyumba vyoote vya nyumba yangu,Walakini USIINGIE CHUMBANI MWANGU maana siku utakapoingia utakufa hakika! " Alafu akaja mtu mwingine akwambie;
" Ati! hivi ndivyo alivyokuambia mwenye nyumba,USIINGIE VYUMBA VYOOTE?"

Chunguza maagizo hayo mawili kwa umakini na utagundua kwamba agizo la kwanza la mwenye nyumba limemruhusu mtu kuingia vyumba vyote isipokuwa chumba kimoja tu,lakini sentesi hiyo ilipoulizwa kwa mara ya pili,kwa mtu huyo mwingine ikapinduliwa kwamba " Ati hivi ndivyo alivyosema mwenye nyumba,USIINGIE VYUMBA VYOTE? Wakati mwenye nyumba hakuagiza hivyo.
Sijui unanielewa hapo?
Hivyo kile kilichomfanya mtu kula tunda la mti aliokatazwa ilikuwa ni Uongo wa ibilisi aliyevaa uhusika wa nyoka,maana yeye ni baba wa huo uongo.
Nyoka aligundua kwamba hana uwezo wa kumdanganya Adamu akadanganyika maana adamu ndie aliyeagizwa na Mungu. Hawa hakuwa na agizo hilo ila amelisikia kutoka kwa Adamu,sababu Adamu alikuwa ni kichwa cha Kristo kwa Hawa,na Hawa alikuwa kichwa cha Adamu.

" Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu." 1 Wakorintho 11:3
Bwana Yesu asifiwe...
Haleluya,nasema jina la Bwana Yesu liinuliwe siku ya leo...

Siku ya leo tunajifunza jambo moja kubwa sana mahali hapa,tunajifunza kwamba ;
* Nje ya uwepo wa BWANA kuna mauti.
*Tena hata nje ya neno la Bwana kupo kujaribiwa na kujaribika.

Haleluya...
Tumeona jinsi gani Hawa alivyodanganywa akadanganyika sababu Hawa hakuwa na mzizi wa Neno la Bwana Mungu. Kwa lugha nyingine,neno la Bwana lilimfikilia kwanza Adamu.Hivyo kwa kulikosa neno la BWANA Mungu kulimfanya Hawa adanganywe hata kudanganyika.
Ndiposa mjaribu akamjia Hawa baada ya kuona Hawa hakuwa na mzizi wa neno la Bwana Mungu.

Tazama hata Bwana Yesu alimshinda mjaribu kwa sababu neno la Mungu lilijaa kwa wingi ndani yake,tunasoma;
" Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,"Luka 4:1
Biblia inasema HALI AMEJAA Roho Mtakatifu.Pale mjaribu aliporusha mishale kwa kumwambia Bwana Yesu "...imeandikwa..."naye Bwana Yesu akamjibu "....imeandikwa...."
Yamkini laiti kama BWANA YESU asingejaa neno,basi angejaribiwa na kujaribika kama vile Hawa.

Baada ya kuokoka tu,ni kulijaza neno la Bwana kwa wingi,ili tunapojaribiwa tusijaribike.Lakini pia tumeona jinsi gani mtu yule yule aliyepewa kazi ya kulima na kutunza bustani ya Edeni ndiye aliyepata adhabu ya umauti mara mbili.
Nasema ndio Adamu wa kwanza alikufa mara mbili.Kwanza alikufa kiroho maana alitolewa nje ya Edeni,na pili Adamu likufa kimwili pia,sababu baada tu ya anguko la dhambi,mauti ikaingia.

Sisi nasi tumeirithi umauti,na hakuna hata mmoja wetu aliyekuwa amepona na dhambi,maana tunasoma;
" Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki. Warumi 5:19
Ohooo!
Kumbe mimi na wewe tulikuwa wafu kwa sababu ya kuasi kwake mtu mmoja

TUFANYEJE BASI?
IKIWA SOTE TUMEHESABIWA DHAMBI!

JIBU;
Ni kujisalimisha kwa BWANA YESU kwa njia ya toba.

Ndiposa Bwana Mungu kwa sababu ya kutupenda mno hata akamtoa mwanaye wa pekee ili kila amwaminie asipotee Bali awe na uzima.
" Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."Yoh.3:16
*Ndiposa Bwana akaja kurejesha na kutafuta kile kilichopotea.
Haleluyaa...
Sasa unisikilize kwa makini sana;
Baada ya anguko,Adamu na Hawa wakafukuzwa bustanini,maana BWANA Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; ( Mwanzo 3:22)

Hivyo akamtoa katika uzima/EDENI.Mtu akatolewa nje ya UWEPONI MWA BWANA,nje ya Edeni.
*Nje ya uwepo wa BWANA kuna mauti,
Kama vile samaki umtoavyo nje ya maji,ni lazima afe.
Maisha ya mkristo hutegemea uwepo wa Bwana Mungu.
Au,
Mfano wa mmea nje ya ardhi,ufa.!
na ndivyo ilivyo mtu nje ya Bwana.

Sasa angalia;
Adamu akafukuzwa atoke nje ya Edeni,maana BWANA MUNGU akasema mtu huyo asije akanyoosha mkono wake akala mti wa uzima akaishi milele(Maana kulikuwa na miti miwili iliyotajwa,mti wa ujuzi wa mema na mabaya,pamoja na mti wa uzima).

Yesu akaja,akawa ni mti wa uzima.
(Yoh.14:6)- Kweli,njia na Uzima

Hivyo kile kilichopotea kimerejeshwa na Bwana Yesu Kristo kwa yeyote yule amwaminiye,tazama asema hivi;
" Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi;
naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki hayo? " Yoh. 11:25-26

Bwana Yesu Kristo kaja na uzima ulee ambao Adamu wa kwanza aliukosa.
Bwana Yesu Kristo yu hai,
YEYE YESU WA NAZARETI NDIO UZIMA WETU.

Nami nakutangazia wewe mpendwa Bwana Yesu yupo muda huu kwa ajili ya kuokoa maisha yako na roho yako,amekuja sasa KUKUOKOA,AMEKUJA NA UZIMA TELE USIOELEZEKA,
Na wala hujachelewa kumpokea,mpokee sasa,
Nipigie simu yangu hii;
0655-111149
Na Bwana atakwenda kukuhudumia.

SAA YA WOKOVU NDIO SASA;
*Kwa huduma ya maombi na maombezi,piga
0655-111149.

MWISHO.

Comments