KUILIMA NA KUITUNZA BUSTANI YA EDENI * sehemu ya tatu *

Nakusalimu katika jina la BWANA YESU;
nikikuambia;

Bwana Yesu asifiwe.
"BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu,akamweka katika bustani ya Edeni,ailime na kuitunza." Mwanzo 2:15
Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla
Ninapozungumzia habari ya kuilima Edeni,hapo huwa ninazungumzia kazi aliyopewa mwanadamu kutoka kwa Mungu aifanye awapo chini ya jua hili.
Zipo kazi nyingi chini ya jua,

lakini kazi hizo si kazi mbele za Bwana Mungu.Kazi ambayo ni kazi mbele za Mungu Baba ,ni kazi ya kuwafungua wale wote walioonewa na ibilisi tena pamoja na kuhubiri injili kwa kila kiumbe.
BWANA Mungu anaitambulisha rasmi kazi moja iliyo njema chini ya jua kwa kinywa cha mtumishi wake Petro akisema;
" habari za Yesu wa Nazareti,jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu;naye akazunguka huko na huko,akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na ibilisi;kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye." Matendo 10:38
Hivyo;
Kazi iliyo njema ni kazi moja tu,ya kuponya wote walioonewa na ibilisi,na kwa Injili kwa kila kiumbe kwa uweza wa jina la Yesu Kristo wa Nazareti pekee. Hakuna kazi nyingine iwayo yote ambayo BWANA Mungu ameithibitisha maana ameona thamani kubwa.

Nami leo hii nasema hakuna kazi nyingine ya kumfurahisha BWANA Mungu kama kazi hiyo,kazi iliyo njema usoni pa BWANA wala si kazi ya uhasibu,
si udaktari,
si uinjinia,
Wala si umakenika!
Bali kazi njema ni kazi ya INJILI YA BWANA KWA KILA KIUMBE.

Leo tunaambiwa twende ulimwenguni mwote tukahubiri injili kwa kila kiumbe(Marko16:15).Kuilima bustani ya Edeni ni kufanya kazi ya Bwana Mungu katika shamba lake.
Kumbuka jambo moja,kwamba;
Mungu hutenda na wanaotenda,hufanya na wanaofanya.
Hata matendo ya mitume iliandikwa kwa sababu mitume walitenda.
Katika agano jipya tunaona Bwana Mungu hakwenda mbele yeye kama yeye bali alikwenda na waliokwenda.
tunasoma;

"Nao wale wakatoka,wakahubiri kotekote,Bwana akitenda kazi pamoja nao,na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo."Marko 16:20
Haleluya...
Nasema haleluya...

Tazama andiko (Mwanzo 2:15),BWANA Mungu akimwagiza mtu,asiishie kulima tu,Bali atunze pia.Yeye alimaye amepewa jukumu la kutunza pia.
02.KUTUNZA EDENI.
Kutunza ni kulinda dhidi na maadui.
Yeye mwenye kutunza kitu,huzuia uharibifu kutoka kwa adui.
Kutunza Edeni ni kulinda uwepo wa kimungu ulio ndani yako usipotee.

Biblia inatuambia kwamba mwili ni hekalu la Roho mtakatifu,ambaye Yeye Roho hukaa ndani yetu,nasi tumepewa bure hii miili ( 1 Wakorintho 6:19)
Hivyo Yeye Roho Mtakatifu akaapo,mahali hapo ni sehemu takatifu yenye UWEPO wa Ki-Mungu.Kwa lugha nyingine mahali halo ni EDENI YA BWANA MUNGU.

Ndiposa tunasoma ya kwamba, BWANA Mungu akamtwaa huyo mtu na kumuweka bustanini ili ailime na KUITUNZA(Mwanzo 2:15).Hapo tunaambiwa tutunze EDENI iliyo ndani yetu.
Hapo zamani kulikuwa na sanduku la agano mahali ambapo BWANA Mungu alikuwa anakaa (1 Samweli 5:1).Lakini leo BWANA Mungu hukaa ndani yako wewe.Hivyo mwili wako ni makao ya Roho Mtakatifu.
Leo unaambiwa umepewa kazi ya KUTUNZA EDNI/KUTUNZA MAKAO YA ROHO MTAKATIFU.

"akamtwaa huyo mtu ailime na KUITUNZA". Mwanzo 2:15
Haleluya...
Groly to God...
Jina la BWANA liinuliwe...

Umepewa mwili huo ulionao hivi sasa sio kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya BWANA (1 Wakorintho 6:13).Mungu anataraji neno lake alilokuambia leo,kwamba; " UJITUNZE "ujitunze kweli kweli.
Kwa nini uchafue mwili wako kwa zinaa?
Tazama pindi unapouharibu mwili wa Bwana,Bwana naye atakuharibu wewe.

" Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu,Mungu atamuharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu,ambalo ndilo ninyi."1 Wakorintho 3:17
Na kama hiyo haitoshi,basi tazama pale Bwana Yesu alipoingia ndani ya hekalu la BWANA kisha akaona biashara zinanoendelea badala ya sala,akaamua kupindua hata meza zao na kuwaambia kwamba nyumba ya Baba yangu ni nyumba ya sala.
Alikadhalika kwako,huo mwili wako sio wa biashara yoyote ile,isipokuwa ni kwa ajili ya BWANA tu.
Leo hii wapo watu waliojiharibu miili yao kwa kujichola chola,wengine wameiharibu miili yao kwa kujiunza.Tena cha kushangaza zaidi;watu wa namna hiyo ni wale wenyekujiita wakristo.
roho yangu huwa inafadhaika sana nionapo watu wa namna hii,maana wanalifanya jina la BWANA kutukanwa,
nami ninaomba;
Ee Mungu achilia rehema zako na neema ya wokovu wako ulio mkuu kwa watu wote walioshindwa kutunza miili yao.

Bwana Yesu asifiwe...
*Kutunza Edeni ni kulinda muujiza wa Mungu ndani yako usipotee.
Tazama pale mtu alipowekwa ndani ya Edeni aitunze,alichokuwa akiambiwa ni kwamba alinde matendo makuu ya BWANA yesipotee kamwe kutoka ndani yake.
• Mimi sijui kama unanielewa vizuri mahali hapa.
• Mungu akusaidie mpendwa ili unielewe.

Yapo mambo mengi makubwa ambayo BWANA Mungu amefanya kwako wewe mpendwa uliyeokoka.
Ipo huduma inayoendelea ndani yako,Tazama;
ulipokuwa mchafu BWANA Mungu alikupokea na kukuosha,akakupa na maisha mapya kabisa kwa kusudi maalumu na lengo maalumu,huo pekee ni muujiza tosha tena ni muujiza mkubwa kuliko yote.

Lakini siku ya leo unaambiwa " KUTUNZA EDENI"yaani; utunze matendo/muujiza huo wa kuoshwa kwa uweza wa damu ya Yesu na kupokelewa mikokoni mwa Bwana Mungu.
Haleluya...
Yapo maagizo ya msingi ndani ya UWEPO wa MUNGU.Ndani ya uwepo wake,tunaona mtu wa kwanza akiambiwa maagizo ya kufanya na ya kutokufanya.
Biblia inasema;

"BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu,akisema,Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula,walakini matunda ya mti wa ujunzi wa mema na mabaya usile,kwa maana siku utakapikula matunda ya mti huo utakufa hakika." Mwanzo 2:16-17
Bwana Mungu anaweka maagizo kwa Adamu na mkewe pia juu ya kutokula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.Kumbuka watu hawa wapo uweponi mwa BWANA Mungu,lakini tunaona bado BWANA Mungu akiwapa MAAGIZO ya kufanya na ya kutokufanya...
ITAENDELEA...
Mpendwa usikubali kuchezea hekalu la BWANA Mungu kwa zinaa,au kwa jambo lolote lile,ukijisikia kwamba unahitaji maombi katika eneo hilo,au eneo lolote lile lilokugusa basi nipigie kwa namba yangu hapo chini ili tuombe pamoja.
Kumbuka;
Wakati wa wokovu ndio sasa,waweza kunipigia na BWANA atakwenda kukuhudumia.

*Kwa huduma ya maombi na maombezi;
piga;
0655-111149.

Usikose fundisho lijalo mahali hapa hapa.
UBARIKIWE.

Comments