KUWEKWA ALAMA YA DAMU YA MWANAKONDOO WA MUNGU ALIYE HAI.* sehemu ya kwanza *

Na mtumishi wa MUNGU Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe....
Heri ya maandalizi ya sikukuu ya Pasaka...
I say again to you;
Blessed be the name of the Lord...
Say;
AMEN...

Ninakukaribisha katika mfululizo wa fundisho hili siku ya leo. Fundisho hili limekujia kwa dhumuni na wakati sahihi kabisa,nami ni matumaini yangu utafaidi sana kwa fundisho hili,raha hizi uzipatazo leo hakikisha usifaidi peke yako,umwalike na mwingine aweze kutembelea mahali hapa pazuri kama nini.

Haleluya...
Tunaanza kwa andiko hili ;

" Kisha akamsongeza kondoo mume wa pili, huyo kondoo wa kuwaweka wakfu; na Haruni na wanawe wakaweka mikono yao kichwani mwa huyo kondoo.

Kisha akamchinja; na Musa akatwaa katika damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la kuume la Haruni, na katika chanda chake cha gumba cha mkono wake wa kuume, na katika kidole cha gumba cha guu lake la kuume.

Kisha akawaleta wana wa Haruni, na Musa akaitia hiyo damu katika ncha za masikio ya kuume, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vya gumba vya maguu yao ya kuume; kisha Musa akainyunyiza hiyo damu katika madhabahu pande zote. " Walawi 8:22-24

Haleluya....

Mpendwa rudia tena kusoma mara nyingine,soma kwa makini kabisa hilo andiko ( Walawi 8:22-23) Maana najua kabisa yamkini hujaelewa ni nini kinachozungumzwa hapo.
OK,
Sasa twende pamoja;
Ukisoma kuanzia mstari wa kwanza wa kitabu cha Walawi sura ya nane,utaona BWANA Mungu akinena na Musa akimpa maelekezo ya kufanya juu ya Haruni na wana wake.

Katika hayo maelezo, Bwana Mungu anamuambia Musa achukue mahitaji ya kukamilisha zoezi alilokuwa akiliendea kulifanya mbele ya Haruni,akimwambia achukue ;
mavazi ya kumvika Haruni,
Mafuta,
Ng'ombe mume wa sadaka ya dhambi,
Kondoo waume wawili, na
Kikapu cha mikate isiyotiwa chachu.

Tena aitishe kusanyiko mahali pa madhabahu ya Bwana,(malangoni pa hema ya kukutania).
Kila hitaji moja lilikuwa na kazi yake ya maana ya kukamilisha zoezi. Mfano ;
Mafuta yalikuwa kwa ajili ya kazi ya kutakasa,
Ng'ombe mume wa sadaka ya dhambi alikuwa kwa ajili ya kazi ya ondoleo la dhambi zao kwa kupitia damu ya ng'ombe huyo.

Ikumbukwe kwamba;
Hapo awali;
Damu ya mnyama ilihusika na kusafisha dhambi.Na ndio maana tunapoona yeyote yule aliyetaka kujitakasa basi alikuwa hana budi kutafuta DAMU ya mnyama.

" Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo." Waebrania 9:22

Damu ya mnyama, ilihusishwa na kuondoa dhambi katikati yao wana wa Israeli,DAMU ilikuwa ni dhabihu.Lakini ukweli ni kwamba DAMU ya mnyama likuwa haiondoi dhambi Bali kufukia dhambi na ndio maana watu hao walihitaji kujisafisha kila mwaka kwa habari ya ondoleo la dhambi. Hivyo toba hiyo ilikuwa ikijulikana kama kumbukumbu la dhambi la kila mwaka
Tunasoma;

" Lakini katika dhabihu hizo liko kumbukumbu la dhambi kila mwaka.
Maana haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi." Waebrania 10: 3-4

Leo hii,DAMU YA MWANAKONDOO WA MUNGU ALIYE HAI ndio damu ya pekee yenye kunena mema,yenye kusafisha na KUONDOA DHAMBI kabisa kabisa,sababu ipo nguvu ndani ya damu ya Yesu Kristo.
I say there is a mighty power in the blood of Jesus,
Say ;
AMEN...

Damu ya mafahali na mbuzi kamwe haziwezi kuondoa dhambi,isipokuwa damu ya mwanakondoo wa Mungu,Damu ya Bwana Yesu Kristo pekee ndio Damu ya msalaba.

Haleluya...
Oohoo Haleluya...
Nampenda Bwana Yesu kwa UWEZA ulio ndani ya damu yake,sijui wewe?

Ok,
Hitaji jingine alilopewa Musa katika zoezi alilokuwa akiliendea kulifanya lilikuwa ni;
*Kondoo waume wawili,
Sikia hii;
Kondoo hawa walikuwa ni wawili ( Walawi 8:2)wenye kazi mbili tofauti.
Kondoo wa kwanza alikuwa ni kwa ajili ya Sadaka ya kuteketezwa mbele za BWANA Mungu.

Kondoo wa pili,ndio damu yake ilitumika kuweka ALAMA kwa Haruni na wana wake.Na kupitia kondoo huyo wa pili,ndie sababisho la fundisho letu siku ya leo kama tulivyosoma hapo juu kabisa ( Walawi 8:22-24)

Soma tena sasa (Walawi 8:22-24)
Baada ya kuchinjwa kondoo wa pili,Biblia inatuambia Musa akatwaa damu ya mwanakoo huyo kisha akapaka katika sikio la kuume la Haruni,kisha akachovya tena damu hiyo hiyo akampaka Haruni katika kidole gumba chake cha mkono wa kuume,kisha akaitwaa tena mara ya tatu na kumpaka Haruni kidole gumba cha mguu wake wa kuume,na kurudia zoezi hili kwa watoto wake Haruni ( Walawi 8:22-24).

Zoezi alilokuwa akilifanya Musa kwa Haruni ni KUMTIA ALAMA YA DAMU YA KONDOO ambaye aliyeelekezwa na Bwana Mungu.

ALAMA NI NINI?
Alama ni ishara ya utambulisho wa jambo au kitu fulani.
mfano;
Wafugaji huwaweka alama mifugo yao,hata pale mifugo yao inapochangamana na mifugo mingine,basi yeye mfugaji huwatofautisha mifugo hiyo kwa sababu ya ile ALAMA.Labda pale waionapo mifugo yao huweza kusema huyu ni wangu na yule si wangu.

Sisi watu wa nyumbani mwa Bwana tumewekewa alama ya chapa ya mwana-kondoo wa Mungu aliye hai.Biblia inasema Musa akampaka Haruni damu ya mwanakondoo,ni sawa na kusema Musa alikuwa AKIMWEKA ALAMA Haruni pamoja na watoto wake wote,kwamba wao ni mali ya Bwana,alikadhalika wewe nawe ikiwa umeokoka basi ujue una alama ndani yako ya damu ya msalaba.

kile alichokifanya Musa katika agano la kale ndicho hicho hicho kinafanana na alichokifanya Bwana Yesu Kristo pale msalabani katika agano jipya.Alipokuwa msalabani alituchora ALAMA ya damu yake ndani yetu.
Sababu Yeye Yesu alifanyika dhabihu ya dhambi ingawa Yeye hakufanya dhambi,alifanyika laana kwa ajili yako wewe na mimi pia tuliokuwa na dhambi,Tunasoma;

" Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;" Wagalatia 3:13

Kuwekwa kwa alama ya damu ya mwanakondoo wa Mungu ilikuwa ni kulipa gharama ya dhambi ndani yako na KUKUTAMBULISHA RASMI kwamba wewe si mali ya ibilisi tena bali ni mali ya Mungu aliye hai.Damu ya mwanakondoo ni damu ya thamani sana kuliko kupita maelezo yawayo yote awezayo kueleza mtu chini ya jua hili nchi idumupo.

" Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;

bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo." 1 Petro 1:18-19

Bwana Yesu asifiwe...

Alama aliyoiweka Bwana Yesu Kristo pale msalabani ilikuwa ni ALAMA ya gharama kubwa,alitununua kwa thamani kubwa sana.
Adui hana uwezo kabisa kuifuta alama zilizokuwepo ndani yetu.

Sisi wakristo tunajulikana kwa alama ya damu ya Bwana Yesu Kristo pekee na si damu nyingine.DAMU hujitambulisha yenyewe pasipo kuitambulisha,na ndio maana mlokole hutambulishwa na nguvu ya damu ya Bwana Yesu,damu ya mwanakondoo alie hai,hata pasipo yeye mlokole kujitambulisha.

Mfano;

Ukiliona gari aina ya Rav-4 barabarani ikipita huku ikiwa imebanduliwa nembo ya Rav-4 na kuwekwa nembo ya gari ya Kolola;
Lakini nakuambia bado watu watainyooshea mkono na kusema;
NEMBO NI YA KOLOLA,LAKINI GARI SI KOLOLA BALI NI RAV-4;
HIVYO,
HILI GARI NI RAV-4,NA WALA SI KOLOLA INGAWA IMEBADILISHWA.
Hata iweje bado watu watasema gari hill ni Rav-4.Kamwe halitajifichi.

Na ndivyo ilivyo kwa mtu aliyepakwa/aliyewekwa alama ya damu ya mwanakondoo,mtu huyu aliye rohoni lakini,akijibadilisha,Lakini bado watu wataiona ALAMA YA DAMU YA MWANAKONDOO NDANI YAKE na kusema mbona wewe umeokoka?

ITAENDELEA...

Usikose kabisa fundisho lijalo mahali hapa hapa.

*Kwa huduma ya maombi na maombezi,piga namba hii;
0655-111149.

UBARIKIWE.

Comments