
BWANA YESU
asifiwe ndugu zangu.
Namshukuru
MUNGU wa mbinguni kwa uzima wake kwangu na kwako pia maana uzima aliotupa MUNGU
ndio chanzo cha sisi kukutana hapa kupitia neno la MUNGU.
Imani ni
muhimu sana kwa kila mkristo kwa sababu mambo yote ya wokovu tunayapokea kwa
imani.
-Mambo ya
uponyaji tunapokea kwa imani.
-Majibu ya
maombi tunapokea kwa imani.
Imani ni
kuwa na uhakika wa mambo unayotarajia, ni mambo yasioonekana lakini kwa imani
huja na kuonekana.
Waebrania
11:1-( Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.
)
-Ukimwendea
MUNGU kwa maombi , au kwa sadaka au kwa chochote, lazima uende kwa imani.
-Hata wokovu
wetu tumeupata kwa imani.
Waefeso
2:8-10 ( Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha MUNGU;
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. )
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika KRISTO YESU, tutende matendo mema, ambayo tokea awali MUNGU aliyatengeneza ili tuenende nayo. )
Imani sio
kipofu, imani inaona, imani ina macho; Na mtu wa imani anaona kabisa kwamba
anapona kweli.
Sura ya
Waebrani 11 inaitwa UKUMBI WA MASHUJAA WA IMANI.
Mwanamke
mmoja alisima katika maombi akitumia
Waebrania 11:35a( Wanawake walipokea wafu wao waliofufuliwa. ), baada ya mme wake kufariki kwa ajali huku huyu mwanamke
akiwa mjamzito. Lakini kwa imani katika maombi , aliomba hadi mme wake akafufuka
baada ya siku 4 akitumia andiko hilo. Maana baada ya siku 4 za maiti yake kuwa
mochwari na hadi kufikia hatua ya kuganda. Siku ya 4 baada ya mwili kuganda kwa
sababu ya kukaa mochwari lakini siku ya 4 Waliibeba maiti na kuipeleka kwenye
mkutano wa Reinhard Bonke, walipofika kwenye mkutano wahudumu waliogopa
kuipeleka maiti mbele ili kuombewa maana mawazo yao yalikuwa je kama
asipofufuka itakuwaje?
Yule mama
kwa imani kubwa alikuwa akiwasisitiza wampeleke mmewe mbele akaombewe lakini
wahudumu waligoma, na kuipeleka nje ya mkutano lakini wakati wa maombezi Nguvu
ya MUNGU ilishuka na yule maiti akaijiwa na uhai maana kwanza wakati maombezi
yakiendelea barafu ilianza kutoka katika
mwili wa ile maiti na baada ya muda yule maiti alisikika akisema ‘’ faili langu
faili langu’’. Kumbe alikuwa mbinguni kwa siku 4 lakini kwa imani mke wake
aliomba na kuomba sana akitumia Hiyo Waebrania 11:35a. N hadi sana ni watumishi
wa MUNGU; na hii ilikuwa ni Nigeria.
IMANI
INANGUVU, IMANI INAONA, IMANI UNAAMINI .
-Ukisimama katika
neno la MUNGU kwa maombi ya imani, MUNGU anatenda kupitia neno hilo.
-YESU KRISTO
ni yeye yule, jana na leo na milele na yote kwake yanawezekana kwa yule mwenye
imani aaminiye.
-Imani ni
kuwa na ufahamu na uhakika wa mambo tusiyoyaona.
KATIKA
IMANI: Unakuwa na uhakika na MUNGU unayemwendea.
IMANI inajua
kwamba MUNGU anaweza yote.
Huwezi
kumpendeza MUNGU kama huna Imani.
MUNGU
awabariki sana kwa tafakali hiyo.
na kama
hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na
atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa
mafundisha kanisani. ROHO MTAKATIFU aliyenipa ujumbe huu ana makusudi kabisa na
wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU
akubariki sana .
Ni mimi
ndugu yako
Peter M
Mabula
Maisha ya
Ushindi Ministry.
0714252292
Comments