MESS JACOB CHENGULA NA MASANJA MKANDAMIZAJI WAZIDI KUPAGAWISHA MKOANI IRINGA

Katika mkutano ulioandaliwa na Mchungaji Chacha eneo la Ruaha Mbuyuni Iringa wazidi kuwa moto moto kutoka na uwepo wa Mungu. Watu wanapata Neno la Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu kwa njia ya mahubiri na nyimbo.

Kulia ni Mess Jacob Chengula na Masanja Mkandamizaji

Mess Jacob Chengula ambaye amefanikiwa kuwa na albamu yake ya MUNGU HABADILIKI aliwasha moto wa ajabu pale alipoingia kwa wimbo wake wa MUNGU HABADILIKI uliobeba ujumbe malidadi sana kwa wana Iringa. Watu walionekana kufurahishwa sana na kufunguliwa kutokana na wingu la Mungu lililofunika eneo hilo.


Mess Jacob Chengula akifanya yake kwa utukufu wa Mungu

Kila siku ninasema, kama wewe unaona kufanya kazi ya Mungu ni ushamba na unapoteza muda, basi Mungu anao wengi sana wa kufanya nao kazi na hata humbabaishi, ila ukibanwa kwa maovu na yeye atakuonea ushamba, maaana ninaamini utaanza kujigonga kwa kumuomba msamaha. Fnaya kazi ya Mungu kama punda hapa duniani ili siku ya mwisho ya kuishi hapa duniani ukaishi maisha ya kifalme Mbinguni kwa BABA.


Masanja Mkasndamizaji akitumia kipaji chake na karama aliyozawadiwa na Mungu siku hiyo


Kumbuka baada ya kumaliza huu mkutano wa Iringa siku ya leo Jumamosi wanaelekea katika mkutano ulioandaliwa na Mwinjilisti Jailos Maloda na Mtume Nyaga wa kanisa la RGC hapa jijini Dar es Salaam unaoenda kwa jina la MOROGORO YOTE KWA YESU

                                   Chanzo: Ruma africa

Comments