MSALABA JUU YA JENEZA LAKO

Na Mwinjilisti John Chinyuli

Sijui kama umeshawahi kuwaza kuwa siku moja ukifa juu ya jeneza lako na kaburi lako utawekwa msalaba,haijalishi unataka au hutaki lakini wenzako watakuwekea alama ya msalaba tu,hawataweka vyeti vyako vya madigri yako au picha ya gari yako au vyeo vyako au chupa ya bia unazokunywaga ok tuendelee,.."swali ninalo taka ujiulize je unao uhusiano wowote na huo msalaba watakao kuunganisha nao,utakao wekwa juu ya jeneza au kaburi lako wewe kama wewe unamahusiano yoyote na huo msalaba"yaani huo msalaba utakao wekwa juu ya jeneza au kaburi lako unasadifu kuwa huyu aliye ndani anahusiana na huu msalaba uliowekwa juu yake au ndio kwanza msalaba unakusaidia kukuhukumu na kuwa kizibiti kwako siku hiyo kuwa msalaba ulikuwepo na wewe ukafuata anasa zako na mambo yako yasiyo mpendeza Mungu.

Msalaba ni Yesu mwenyewe,msalaba ni zaidi ya ile alama,msalaba ni ngazi ya kupandia mbinguni,ipo nguvu ndani ya msalaba,maneno ya Mungu yanasema "Mtu yeyote akitaka kunifuata ajikane mwenyewe,ajitweke msalaba wake,anifuate" 'Mark 8:34' 

 angalia hayo maneno 'ajikane mwenyewe' na 'ajitwike msalaba wake' kumbe basi ili tuwe tumeunganishwa na msalaba kiuhalali ni lazima tujikane wenyewe nafsi zetu na yale mambo yanavutia kwa macho ya anasa katika dunia hii ya leo inayovuta mno kwenda jehanamu kuliko mbinguni na kila aina ya maovu yafurahishayo nafsi(ile kitu moyo unapenda) yatupasa kuachana nayo na kila aina ya mikumbo ya watu ambao wamesha ahirisha kwenda Mbinguni yatupasa kuachana nao kama tu tutahitaji tu misalaba itakayo kuwa juu ya majeneza na makaburi yetu isadifu kilichobebwa ndani kuwa aliye zikwa au aliye wekwa ndani ya kaburi hili aliubeba msalaba au aliutupa na kufuata mambo yake mwenyewe(anasa) unaweza kusema roho itakuwa ishaondoka ndio ninakozungumzia huko huko sasa roho itakapo kuwepo maana kuubeba msalaba ni kumbeba Yesu mwenyewe mioyoni mwetu na nini basi maana ya kumbeba Yesu mioyoni mwetu yaani maisha yetu yawe ya haki yasiyo na uchafu wowote wa dhambi maana kumbeba Yesu ndio mafanikio yenyewe katika kila jambo na maisha ya dhambi ni hasara na uharibufu mtupu,hata hivyo Kristo Yesu aliangikwa msalabani ili kutuunganisha sisi na Mungu kwa kile kifo chake msalabani ila pale tu utakapoamua kufuata vile yeye atakavyo nadhani unazifahamu sera zenyewe moja wapo ni KUACHA DHAMBI na hapo ndipo unakuwa amekuunganisha na Mungu yaani unakuwa unaurithi uzima wa milele na si Jehanamu ya moto na ndio maana basi juu ya Jeneza au kaburi huwekwa msalaba,mtume Paulo akasema"kwa sababu neno la msalaba kwao wanao potea ni upuuzi,bali kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu ya Mungu" 1kor 1:18 

.kumbe basi habari za msalaba ni za maamuzi ya mtu tena maamuzi binafsi yenye msimamo ndani yake yakwamba kuona thamani na uhitaji wa kuishi maisha ya Haki kwa sababu ya msalaba na ndipo nguvu za Mungu huwa juu yake na nguvu za Mungu ndio ushindi wenyewe,kustawi,kulindwa,kumshinda shetani,Baraka,uponyaji,kufaulu,furaha na utoshelevu maishani ili siku moja msalaba usije kusema haukuji au uliuona msalaba kama upuuzi mtupu kutokana na njia zako unazozifanya unafanya dhambi kwa siri eti kwa ajili watu hawakuoni na jamii imekuamini basi umeamua kuishi maisha ya kishetani umezoea na huoni hofu umeutupa msalaba heiiii amua sasa KUFANYA MAAMUZI MAGUMU ya kuacha dhambi maana unajiandalia uharibu maishani mwako ambao gharama za huo uharibifu zitakutesa na hutaweza kuzisitahimili,MPE YESU MAISHA LEO.  

                        MUNGU akubariki sana.
 
                 By Mwinjilisti John Chinyuli 
                 0767 592989/0712 592989

Comments