MTOTO ALIYEPIGWA RISASI YA KICHWA KANISANI, APEWA RUHUSA YA KUTOKA HOSPITALINI BAADA YA MATIBABU


Mtoto Satrine akiwa na baba yake hapo jana, baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini ©mobile.nation
Hatimaye mtoto wa mwaka mmoja na nusu Satrine Osinya ambaye risasi ilituhama kichwani kwake baada ya tukio la mtu asiyefahamika kuvamia kanisa mjini Mombasa na kufyatua risasi na kuua watu wawili eneo la tukio na wengine wanne baadae akiwemo mama mzazi wa mtoto huyo, hapo jana ameruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa chini ya uangalizi wa daktari baada ya kutolewa risasi hiyo.

Mtoto Osinye alifanyiwa upasuaji tarehe mosi ya mwezi huu katika hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi nchini Kenya kisha kuwekwa chini ya uangalizi ambapo hali yake imeendelea vyema na kuanza kucheza kama ilivyo kwa watoto wengine hali ambayo imeonyesha hali yake iko salama hivyo madaktari kumpa ruhusa hapo jana.

Picha ya mama mzazi wa mtoto huyo, ikiwa juu ya jeneza wakati wa mazishi wiki iliyopita.

Kama hukusoma habari ya risasi ilivyotokea BONYEZA HAPA habari kwa hisani ya NTV



Chanzo ni Gospel kitaa

Comments