WATU 200 WAOKOKA KATIKA SIKU YA 3 YA MKUTANO WA MTUME PETER NYAGA MOROGORO.


"Morogoro Yote kwa Yesu" huo ndio usemi unayotamba sasa mkoani Morogoro kwa sasa, watumishi wa Mungu wameandaa mkutano huu wa kumtangaza Yesu Kristo na kuwafungua watu waliofungwa na mateso mbalimbali. Siku ya Jumapili watu walimimika katika eneo la tukio kushuhudia jinsi gani Mungu anafanya makuu kwa kupitia watumishi wake waliopo hapa dunia. Watu wenye mapepo walionekana kugalagala chini wakihangaika na kulia kwa maana mapepo yalikuwa yakiunguzwa moto wa Yesu Kristo. Hakika watu wa Morogoro sasa wanajivunia ohuyu Bwana Yesu kwa hale hyaliyotokea jana na yatakayoendelea kutokea kwa kipindi kizima ambacho watumishi hawa wa Mungu watakuwa wanafanya kazi ya Mungu.
Katika mkutano wa jana jumapili watu 200 waliokoka na kuanzia sasa ni wateule wa BWANA YESU waliosafishwa kwa damu yake takatifu.
UTUKUFU KWA MUNGU.
Mtume Peter Nyaga

Mtume Peter Nyaga wa kanisa la RGC Tabata Chang'ombe Dar es Salaama ameacha kanisa lake kwa lengo la kuja kuwasaidia hawa watu wa Morogoro walioteseka kwa muda mrefu kwa magonjwa na taabu mbalimbali, wametumikishwa na shetani vya kutosha. Wewe uliye Morogoro na mikoa ya jirani fika katika eneo la tukio upokea muujiza wako.



 




Comments